Pamoja na wenyewe kudai hawajui kilichotokea, mastaa wawili wenye
sura za mauzo kunako sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Wema
Isaac Sepetu, kwa sasa wanadaiwa kufikia pabaya kufuatia bifu zito
linalofukuta kati yao.
Habari za mjini zinadai kwamba, Wema amekuwa akishtushwa na kuchukizwa
na kitendo cha Lulu kuwa upande wa aliyewahi kuwa mwandani wake, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ kiasi cha kwenda nyumbani kwake, Madale-Tegeta
jijini Dar, usiku wa manane na kujiachia na jamaa huyo anavyotaka.
“Kama mtakumbuka, kabla ya kifo cha Kanumba (Steven), Wema na Lulu
walikuwa ni mashosti kama ilivyokuwa kwa Wema na Snura (Mushi) au Wema
na Kajala (Masanja) au Wema na Aunt (Ezekiel).
“Lakini baada ya jamaa (Kanumba) kuondoka na kisa kizima cha Lulu ndipo
Wema akavunja urafiki na Lulu kwa sababu Kanumba aliwahi kuwa ‘mtu’ wa
Wema kama ilivyo kwa Diamond.
“Ulipita ukimya wa muda mrefu bila Wema na Lulu kuwa mashosti zaidi ya salamu.
“Lakini mambo yalianza tena kuwa mabaya baada ya Lulu kumponda Wema
alipokuwa akigombea Ubunge wa Viti Maalum kupitia CCM (Chama Cha
Mapinduzi).
“Sasa hivi ishu ni kitendo cha Lulu kujiachia na Diamond kwenye birthday
ya Rome Jones (binamu na DJ wa Diamond) kisha ile pati ya birthday
Diamond kuifanyia nyumbani kwake huku (Lulu) akitupia picha za mafumbo
yaliyoelekezwa kwa Wema.
“Hicho ndicho kinachoendelea na unaambiwa hali ni tete mno,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao.
Baada ya kupata ‘ubuyu’ kamili, Amani lilimtafuta Wema na kummwagia data
ambapo alionesha kushtushwa na kudai kwamba hata yeye anashangaa ni
nini kimetokea.
Kwa upande wake Lulu hakupatikana hewani lakini kwa mujibu wa mahojiano
aliyofanya hivi karibuni juu ya uhusiano wake na Wema, mwanadada huyo
alikiri kuwa rafiki wa Wema kitambo hicho lakini akasema hajui ni nini
kilichotokea zaidi ya kwamba huwa wanasalimiana tu wanapokutana.
Kabla ya mambo kwenda mrama, Lulu na Wema walikuwa mashosti wakubwa
ambapo gazeti hili liliwahi kuwashuhudia wakiwa lokeshi na kulala pamoja
chumba kimoja kama mtu na dada au mtu na mdogo wake.
Chanzo: GPL
Ijumaa, 16 Oktoba 2015
Home »
» LULU, WEMA WAFIKA PABAYA..KISA UHUSIANO NA DAIMOND ..
LULU, WEMA WAFIKA PABAYA..KISA UHUSIANO NA DAIMOND ..
Related Posts:
EDWARD LOWASSA AMPONGEZA RAISI JOHN POMBE MAGUFULI Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kuondoa urasimu katika taasisi za serikali na kusema hiyo itasaidia kurejesha utendaji kazi kwa ufan… Read More
GAVANA BOT AFICHUA SIRI YA KILIO CHA FEDHA KUPOTEA MTAANI Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa.Akizungumza na waa… Read More
CONGO DRC: WAASI WA MAI MAI WAMEWATEKA MADEREVA 5 WA TANZANIA, WANATAKA $ 4,000 KWA KILA DEREVA KUNA TAARIFA KUWA waasi wa Mai Mai wamewateka madereva wa Tanzania watano na kuchoma baadhi ya magari. Wanadai usd 4000 kwa kila Dereva amasivyo watawapiga risasi. Wametoa deadline ya majeshi kuondoka pia.Chama cha … Read More
DADA WA DAIMOND ESMA PLATNUMZ AKIRI KUMPENDA SANA PETIT MAN AWAOMBA NYAKU NYAKU WASIMNYAKUE Dada wa Diamond ameamua kufunguka ya moyoni na kudai anampenda sana mume wake Petit Man ambae walitengana kwa muda kutokana na kutokuelewa hapa na pale lakini kwa sasa inaonekana wameweka mambo sawa...Ameandika haya… Read More
NAMANGA: EDWARD LOWASSA ASIMAMISHWA NA WANANCHI WAMWELEZE UGUMU WA MAISHA Mh Edward Lowassa Mjumbe wa kamati kuu wa chama Cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA ) na Chama kikuu cha Upinzani TANZANIA na Waziri Mkuu mstaafu amesimamishwa na Wananchi wa Namanga Mpakani mwa Tanzania na Kenya … Read More
0 comments:
Chapisha Maoni