Siku moja baada ya kutangaza kujitoa CCM, kada mkongwe wa chama hicho,
Balozi Juma Mwapachu amesema uamuzi alioufanya ni sahihi ambao hata Baba
wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere angekuwa hai angeufanya kwa sasa.
Balozi Mwapachu alieleza hayo jana katika mahojiano maalumu na kuongeza
kuwa chama chake cha zamani kimepoteza mwelekeo kwa kuwa kinara wa
kuvunja katiba na taratibu kitendo ambacho Nyerere alikichukia katika
maisha yake.
Alisema anafahamu fika kuna watu watakosoa uamuzi wake huo lakini
hatababaishwa na maneno yao na atasimamia msimamo wake huo huku akieleza
kuwa anajisikia amani kujitoa katika siku ya kumbukumbu ya miaka 16 ya
kifo cha Nyerere.
Mwapachu alitangaza kujitoa CCM juzi akisema kilivunja taratibu wakati
wa mchakato wa uteuzi wa mgombea wa urais uliofanyika Julai ambao Dk
John Magufuli alichaguliwa.
“Nimefanya makusudi kujitoa wakati huu kwa sababu hata Nyerere mwenye
angekuwapo hai leo hii angefanya uamuzi kama niliofanya. Hata yeye
alikuwa ameshachoshwa na chama chake kwa uvunjaji wa kanuni, taratibu na
katiba na alikwishaona kuwa kinaanza kupitwa na wakati.”
Alisema mengine yanayojitokeza kwa sasa ndani ya CCM yanaonyesha bayana
kuwa chama hicho hakiendi na wakati na kilijisahau na kuendesha mambo
kama kipo kwenye mfumo wa chama kimoja wakati ni wa vyama vingi.
Alisema CCM ya sasa siyo ile aliyojiunga nayo akiwa chuo kikuu, ndiyo
maana amejitoa kutokana na kutekwa na watu wachache ambao humpiga vita
mtu ambaye si mwenzao.
Ijumaa, 16 Oktoba 2015
Home »
» BAADA YA KUJITOA CCM BAKOZI JUMA MWAPACHU ATOA MPYA..ADAI HATA NYERERE ANGEKUWEPO ANGEJITOA CCM
BAADA YA KUJITOA CCM BAKOZI JUMA MWAPACHU ATOA MPYA..ADAI HATA NYERERE ANGEKUWEPO ANGEJITOA CCM
Related Posts:
ESCROW:Spika adaiwa kuwalinda washukiwa Spika wa bunge la Tanzania Anne Makinda Speaker wa Tanzania Anne Makinda ameshtumiwa kwa k… Read More
Walichokisema Wabunge Kafulila, Peter Msigwa, Aeshi Hilary na Maige kuhusu maamuzi ya Bunge jana Kikao cha Bunge la Tanzania kilichoahirishwa siku ya jana Novemba 29 ni moja ya vikao ambavyo vilivuta hisia za watu wengi na kutengeneza historia nyingine mpya kutokana na mjadala wa ishu ya Escrow, baada ya kikao hich… Read More
Man U na Arsenal zawika,Chelsea yazuiwa Mchezaji wa chelsea Wiilian akikabiliana na mwenzake wa Sunderland Mkufunzi Gus Poyet aliihangaisha timu ya Chelsea na kuwajaribu viongozi hao wa Ligi kupi… Read More
FIFA:Madai mapya ya ufisadi yazuka Rais wa FIFA Sepp Blatter akimkabidhi rais wa Urusi Vladmir Putin Haki za kuandaa dimba la dunia la mwaka 2018 Madai zaidi yameibuka kuhusu ufisadi uliofanyika wakati wa shughuli ya kuwatafuta waandalizi wa … Read More
Obama na vurugu za Marekani &nb… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni