Ijumaa, 6 Novemba 2015

Edward Lowassa/Zitto Kabwe Wapeleka Kilio CCM

Hawa jamaa wawili kwa kweli kwa pamoja tunaweza kusema wamepeleka kilio mtaa wa Lumumba, waswahili husema kwa mjinga huenda kicheko lakini kwa mwelevu huenda kilio.

Ujio wa Lowassa UKAWA umepeleka kilio kikubwa sana CCM japo kuwa wanajikazakinyasa wanakufa na Tai shingoni. Majuzi Mh. January Makamba aliita waandishi wa habari na kujinasibu eti CCMimepata wabunge 176 mpaka sasa na kufanikiwa kugomboa majimbo 11 yaliyokuwa yawapinzani.

Sasa habu ona hapo chini kilio Lowassa alichokipeleka CCM ambacho Makamba hakupenda kutaja.

1. Viti maalumu vya CCM vimepungua kwa 40% toka 79bunge lilopita la10 mpaka 62 bunge la11. Wakati CHADEMA na CUF viti hivyo vimeongezeka haya ni maumivu makubwa

2. CCM imenyang`anywauongozi wa majiji 4 kati ya majiji 5imebakiwa na uongozi katika jiji moja tu la Mwanza,. Majiji yafuatayo CCM nichama cha upinzani , Jiji la Mbeya, Jiji kuu la Dar-es-Salaam, Jiji la kitaliila Arusha na jiji la Tanga ambalo ilikuwa ni ngome yao, ngome imevunjwa.

3. Ruzuku ya CCM imepungua kwa 40% kutokana na kuraza rais alizopata , mgao wa ruzuku utakuwa 60 kwa 40 kwa maana 58% alizopataRais Magufuri kwa desilimali ya karibu itakuwa 60, na 39.8% ya kura za Lowassaalizopata kwa desilimali ya karibu itakuwa 40. Kwa hiyo CHADEMA imeinya`anyaCCM 20% ya ruzuku, je! Siyo maumivu hayo?

4. Uongozi wa halmashauri ndiyo usiseme. Kabla yaLowassa halmashauri zilizokuwa zinaongozwa na wapinzani zilikuwa 5 sasahalmashauli hizo zimeongezeika na kufika 30, katika halmashauri hizo CCMwatakuwa bachbancher.

5. Kilio kikubwa zaidi ni cha Zitto Kabwe alichowapaCCM katika halmashauri ya Kigoma/ujiji. Katika halmashauri hii hakuna mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa kutia pua, halmashauri hii ni mali ya Zitto Kbakwe kwamaana ya Meya hadi madiwani. Halmashauri hii mwenyekiti wa CCM au mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa wataenda kufanya nini? Wakati wakuu hao wameng`ang`anakumnyang`anya Kafulila ubunge wake huku nyuma Zitto anachukua halmashauri ya mjini,shame on them

6. Kuna kilio manispaa ya Mtwara/Mkindani na Mtwaravijijini kwa Hawa Ghasia, huenda Umeya wa Shilingi na wa Ndazigula umeotambawa.

Haya ndo ilitakiwa Mh. January Makamba ayaseme katika kile kikao chawaandishi wa habari alichokiitisha.

Source: ebaeban/Jamii Forums

0 comments:

Chapisha Maoni