Kinyume na ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari Hajaonekana 
kwenye sherehe za kupishwa kwa Mh. Rais na wala jina Lake halikuwemo 
kwenye orodha ya wageni.
Hivi majuzi muhubiri maarufu kutoka nchini Nigeria TB Joshua aliwasili 
nchini kwa kile kilichoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo 
gazeti la Mwananchi kwamba muhubiri huyo amekuja nchini kushuhudia 
kupishwa kwa Rais Dr. John Pombe Magufuli.
Alipowasili uwanja wa ndege hapa Tanzania alipokelewa na baadhi ya 
viongozi walioongozwa na Dr. John Pombe Magufuli na akaenda moja kwa 
moja kumsalimia Rais Kikwete Ikulu magogoni Dar es Salaam.
Baada ya kutoka Ikulu muhubiri huyo alielekea nyumbani kwa aliyekuwa 
mgombea urais wa UKAWA na waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa eneo 
ambalo ameonekana kuwepo kwa Muda mrefu akizungumza na Lowassa na 
viongozi wengine wa UKAWA.
MASWALI
1. Je, ujio wa Muhubiri huyo ilikuwa ni msafara binafsi Kinyume na ilivyoripotiwa na vyombo vya habari?
2. Vyombo vyetu vya habari havikupewa taarifa sahihi kuhusu sababu za ujio wa kiongozi huyo?
3. Kama ni msafara binafsi kwanini apokelewe na rais mteule na kutembelea Ikulu?
4. Je ni viongozi wa UKAWA wamemzuwia kuhudhuria sherehe hizo za kupishwa Rais kutokana na wao kugomea kusaini matokeo?
5. Je, bado yupo nchini? Maana kama tulijulishwa kuhusu ujio wake si vibaya tukajuzwa kuhusu kuondoka kwake.
Nawasilisha:
Ijumaa, 6 Novemba 2015
Home »
 » TB Joshua ni Mgeni wa Nani Nchini Tanzania? Maswali Yazidi Baada ya Kutoonekana Uwanja wa Taifa Katika Sherehe za Kuapishwa







 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni