Tanzania bado iko kwenye majonzi baada ya msiba wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa,Deo
Najua kuna watu walikuwa na maswali juu ya atakayewaongoza wakazi wa 
Ludewa, sasa leo Novemba 5, 2015 mke wa marehemu Deo Filikunjombe ‘ 
Saraha’ ameyaandika maneno haya kupitia akaunti yake ya instagram 
kuhusiana aliyeteuliwa kugombea jimbo la Ludewa.
‘Nawaombeni wana ludewa wote kwa heshima nawaomba niwaambie ukweli 
kuwa huyu ndie anayeweza kuvaa viatu vya mume wangu mpendwa kwani mara 
nyingi amewahi kumchangia kaka yake ada za watoto tuliokuwa 
tunawasomesha huko ludewa naombeni msidanyike na maneno ya hao wagombea 
wengine mbona leo ndo wamekuja ludewa walikuwa wapi kujakuleta maendeleo
 mpaka iwe baada ya deo kufariki kati ya wagombea wote hakuna rafiki wa 
mume wangu’ – Saraha
‘hata mmoja tena kwa macho yangu nimewaona wakipewa misaada walete 
Ludewa na hawakufikisha na mara nyingi amelalamika na kuwaomba jamani 
tupeleke maendeleo nyumbani hakuna aliesikia hata mmoja ndo maana hawana
 nyumba ya kufikia matokeo yake wanawaomba kura ilingali hata hawana 
pakufikia wamefikia nyumba ya kulala wageni mkitaka kumwona mbunge mta 
mkuta wapi tuwemakini Deo amefanya mengi mpeni mdogo wake amalizie 
aliyoahidi asanteni sana wanaludewa niwaganili sana mdalikhe sana ccm 
hoyeeeeeeechagua ccm chagua Philipo filikunjombe hapa kazi tu’ – Saraha
Ijumaa, 6 Novemba 2015
Home »
 »  Mke wa Deo Filikunjombe Ampigia Kampeni Mdogo wa Filikunjombe Achukue Ubunge Jimbo Aliloliacha Mmewe..Adai Wengine Msiwasikilize Hawana Hata Mahali pa Kufikia Ludewa







 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni