Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia Bungeni,
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai kuwa bado
hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya Escrow.
Ahadi
hiyo ilitolewa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika
katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Handeni, akimnadi Daudi Lusewa.
Alisema
baadhi ya mawaziri, akiwamo Muhongo, bado hawajasafishwa na tuhuma za
rushwa zilizosababisha wajiuzulu hivyo wajiandae kwani wabunge wa chama
hicho wamejiandaa kumwangusha.
Mnyika
alisema amemshangaa kuona Rais John Magufuli akimteua Muhongo kwenye
Wizara ile ile alikopatia kashfa, iliyosababisha Rais mstaafu Jakaya
Kikwete kumtema kwenye Baraza la Mawaziri.
“Hatukubaliani
na uteuzi wa Profesa Muhongo na namhakikishia bungeni patachimbika,”
alisema Mnyika ambaye ni Mbunge wa Kibamba, Dar es salaam.
“Hoja yetu ya kwanza tutakapoingia bungeni tu itakuwa kushinikiza Waziri huyu ajiuzulu maana bado hajasafishwa,” alisema Mnyika.
Jumatatu, 14 Desemba 2015
Home »
» Chadema Bado Hawajakubali Yaishe...Waapa Kumshughulikia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Bungeni
0 comments:
Chapisha Maoni