Jumatatu, 14 Desemba 2015

Diamond Platnumz na Zari Washinda Tuzo Nchini Uganda

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ pamoja na mchumba wake Zarinah Hassan ‘Zari The Bossy Lady’ wamepata Tuzo za Abryanz Style and Fashion (ASFA 2015) zilizofanyika Kampala, Uganda usiku wa kuamkia leo.Wawili hao wameibuka kidedea katika kipengele cha East Africa Most Stylish Couple.

Mbunifu wa mavazi, Martin Kadinda naye ameibuka kidedea katika tuzo hizo kwa kipengele cha Mbunifu Bora wa Mwaka huku Mwanamitindo Bora wa Mwaka ikienda kwa Mtanzania mwingine, Dax Hannz.

Mbali na hao, pia Tanzania imepata tuzo kupitia staa wa kike wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee aliyepata katika kipengele cha East Africa’s best Dressed Female Artist.
Katika sherehe hizo zilifunikwa kwa shoo kutoka kwa mkali kutoka Nigeria, Banky W akishirikiana na bidada kunako Bongo Fleva, Linah.

0 comments:

Chapisha Maoni