Mshauri mkuu wa ikulu ya White House kuhusu usalama wa taifa Michael
Flynn amejiuzulu kuhusiana na uhusiano wake na maafisa wa Urusi, vyombo
vya habari Marekani vinaripoti.
Bw Flynn anadaiwa kujadili vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi akiwa na
balozi wa Urusi kabla ya Rais Donald Trump kuingia madarakani.
Anadaiwa kuwapotosha maafisa wa utawala huo mpya kuhusu mazungumzo yake na balozi huyo.
Awali, vyombo vya habari Marekani viliripoti kwamba Wizara ya Haki
ilitahadharisha ikulu ya White House mapema kuhusu mawasiliano ya Flynn
na maafisa wa Urusi mwishoni mwa mwezi uliopita.
Walisema Bw Flynn huenda akashurutishwa kuwa kibaraka wa urusi.
Maafisa wakuu wa chama cha Democratic walikuwa wametoa wito kwa Bw Flynn kuachishwa kazi.
Mashirika ya habari ya Associated Press na Washington Post yanasema
wizara ya haki Marekani ilitahadharisha kuhusu kile ilichosema ni mambo
aliyoyasema Bw Flynn kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi.
Ni kinyume cha sheria kwa raia wa kawaida kujihusisha na shughuli za kidiplomasia Marekani.
Mazungumzo kati ya Flynn na balozi wa Urusi yanadaiwa kufanyika mwishoni
mwa mwaka jana, kabla ya Bw Flynn kuteuliwa kuhudumu katika uatawala wa
Bw Trump.
Bw Flynn, ni luteni jenerali mstaafu.
Awali alikana kuzungumza kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi na balozi huyo,
na Makamu wa Rais Mike Pence pia alijitokeza hadharani kumtetea.
Bw Flynn baadaye aliambia maafisa wa White House kwamba kuna uwezekano yeye na balozi huyo walizungumzia vikwazo hivyo.
Gazeti la Washington Post lilisema Kaimu Mwanasheria Mkuu Sally Yates
aliambia White House kwamba mshauri wao mkuu wa usalama wa taifa
"alijiweka katika hali ya hatari" kwa kuzungumza na Warusi kabla yake
kuruhusiwa kisheria kufanya hivyo na kwamba Wizara ya Haki ilifahamu
kwamba alimpotosha Bw Pence.
Mwezi uliopita, Bi Yates alifutwa kazi na Bw Trump kwa kukataa kutetea
marufuku yake dhidi ya raia wa mataifa saba yenye Waislamu wengi
kuruhusiwa kuingia Marekani.
Jumanne, 14 Februari 2017
Home »
» Mshauri wa Rais Donald Trump Ajiuzulu
Mshauri wa Rais Donald Trump Ajiuzulu
Related Posts:
POLISI MATATANI KWA KUOMBA RUSHWA YA MILIONI 7 POLISI mkoani Rukwa inawashikilia askari wake wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Nkasi, wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh milioni 7.2 wamsaidie mtuhumiwa. Kaimu Kamanda wa Polisi wa Rukwa, Leonce … Read More
Pichaz: Mabusu ya Gigy Money kwa Idris Zawatoa Povu Mashabiki wa Wema Sepetu Picha zinazomuonesha Gigy Money wakati akimpiga mabusu Idris Sultan wakiwa katika show ya Pool Party iliyofanyika Ijumaa iliyopita katika hotel ya Regency Park jijini Dar es salaam, zinawatoa povu mashabiki wa Wema Sepetu. P… Read More
IMF: Uchumi wa Tanzania waongoza Afrika Mashariki Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF. Katika ripoti yake iliyoto… Read More
JISNI YA KUMTAMBUA ASIYE NA MAPENZI YA KWELI Inawezekana upo katika uhusiano na tapeli wa mapenzi bila kujua, hiyo ni sumu na unachotakiwa kufanya sasa ni kuanza kumchunguza mpenzi wako mapema usije ukawa miongoni mwa walio katika foleni! Hakuna kitu kibaya kama kuwa k… Read More
SUMAYE:NASHANGAA KWA NINI RAIS MAGUFULI ANAPENDA SIFA FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais John Magufuli kupenda kusifiwa zaidi na kuchukia kukosolewa, Sumaye bila kumtaja jina Rais Magufuli ameleza kushangazwa na hatua ya serikali ku… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni