Ijumaa, 16 Septemba 2016

ZOMBE AACHIWA HURU, MSHIRIKA WAKE AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA


Mahakama ya Rufaa imemhukumu aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni kunyongwa hadi kufa katika kesi ya vifo vya wafanyabiashara wa madini iliyokuwa ikimkabili yeye pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na maofisa wenzake wawili.

Katika hukumu hiyo, Zombe na maafisa wengine wawili wameachiwa baada ya kushinda rufani hiyo dhidi yao.

Hukumu hiyo imehitimisha mvutano wa muda mrefu wa kisheria kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na maofisa hao kwani baada ya kimya kirefu hukumu hiyo imetolewa.

Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Hukumu hiyo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu, wakiwamo ndugu wa marehemu hao, wanasheria na jamii kwa jumla baada ya miezi minne, majuma mawili na siku mbili, tangu rufaa iliposikilizwa.

DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaachia huru Zombe na wenzake wanane katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wawili wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva wa teksi, mkazi wa Dar es Salaam.

Katika kesi ya msingi, Zombe na wenzake walidaiwa kuwaua kwa kukusudia wafanyabiashara Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, aliyekuwa dereva wa teksi wa Manzese.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.

Agosti 17, 2009, Mahakama Kuu iliwaachia huru washtakiwa hao ikisema baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za mawakili wa pande zote iliridhika kuwa hawakuwa na hatia ya mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Badala ya kosa la mauaji ambalo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufaa, DPP aliiomba Mahakama imtie hatiani Zombe kwa kosa la kuwalinda wahalifu, ambao adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka saba jela.

Wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Timon Vitalis alidai DPP alifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani Zombe kwa kosa la mauaji.

ALICHOKIZUNGUMZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI CONGO KUHUSU MADEREVA WALIOTEKWA


Jana ziliripotiwa habari za kutekwa kwa madereva wa malori kutoka Tanzania na Kenya kutekwa na kundi la waasi nchini Congo. Leo September 16 habari zilizoripotiwa na BBC Swahili zimedai kuwa watu wameokolewa na jeshi la nchi hiyo.

BBC imezungumza na waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo ambapo kuwa madereva wote wameokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo na wako salama. BBC imesema utekaji wa madereva hao ulifanywa na watu wenye silaha katika kijiji cha Matete kuelekea Namoya kilichopo Mji wa Kivu Kusini Mkoa wa Manyema.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Congo alipoongea na BBC kwa njia ya Simu, amesema ni magari saba ya kampuni ya Simba inayomilikiwa na mfanyabiashara Azim Dewji kutoka Tanzania ndio yaliyochomwa.

Waziri huyo amesema tukio hilo halijafanywa na waasi kama ilivyoanza kuripotiwa, ila ni majambazi tu ndio waliofanya tukio hilo.

>>>Ni majambazi tu wanatoka porini walipoona magari yanatembea wakayasimamisha katikati ya pori na kuangalia kama kuna pesa wanyang’anye lakini hawakukuta pesa wakaamua kuwachukua madereva na kukimbia nao porini kisha wakayachoma magari 6 na moja halikuteketea.:- Waziri Mambo ya Ndani Congo.

MAJAMBAZI, MALI ZA WIZI NA SILAHA VYAKAMATWA DAR



Kikosi maalum cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 5 wa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali.

Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Saimoni Sirro akionesha baadhi ya vifaa vilivyokamatwa.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Kamishna Saimoni Sirro wakati akitoa taarifa ya kukamatwa majambazi wa 5 na kukutwa na silaha aina ya shotgun, bastola 3 na risasi 49.

Katika tukio lingine Polisi mnamo tarehe 5.9.2016 majira ya saa 8 usiku maeneo ya Magomeni mtaa wa Makumbusho waliokota begi lililokuwa na bastola mbili, sambamba na hilo wamefanikiwa kukamata magari 4 ya wizi, hati za magari na watuhumiwa wawili wa uhalifu huo wamekamatwa.
Jeshi hilo limetoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa kupitia kamati za ulinzi wa mitaa kuimarisha ulinzi na kuwataka wamiliki wa nyumba za kupanga kuhakikisha wanaweka kipengele cha kuwepo na picha katika mikataba ya kupangisha nyumba zao kutokana na uwepo wa wimbi la uhalifu.

Wakati huo huo Kamanda Sirro amesema Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kipindi cha siku 11 wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 882,570,000 ikiwa ni tozo za makosa ya usalama barabarani na makosa mengineyo.

KUTOKA BUNGENI: RAISI MAGUFULI KUHAMIA DODOMA RASMI MWAKA 2020



Leo Septemba 16, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa nne kwa Bunge la 11 uliodumu kwa muda wa wiki mbili, amesoma ratiba ya serikali kuhamia Dodoma.

“Ili kufanikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma, tayari imeandaliwa ratiba itakayowezesha Serikali kuhamia Dodoma kwa awamu, kuanzia mwezi Septemba, 2016 hadi mwaka 2020, bila ya kuathiri bajeti yetu ya mwaka 2016/2017 kama ifuatavyo”–


1. Septemba 2016 – Februari 2017.

Waziri Mkuu na Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Manaibu Makatibu Wakuu wote watahamia Dodoma katika Awamu ya Kwanza. Aidha, kila Wizara itatakiwa kuhamisha Watumishi wa Idara moja au mbili, na wakati huo huo kuendelea kuweka utaratibu wa kupeleka Watumishi wa Idara nyingine kuhamia Dodoma;

2. Machi 2017 – Agosti 2017.

Kipindi hiki kitawapa fursa watendaji wa wizara mbalimbali kuweka katika Bajeti zao za mwaka 2017/2018 gharama za kuendelea kuhamisha watumishi wake kuja Dodoma.

3. Septemba 2017 – Februari 2018.

Katika awamu hii, Wizara zitaendelea na uhamishaji wa Watumishi wa Idara zilizo ndani ya Wizara.

4. Machi 2018 – Agosti 2018.

Katika kipindi hiki, Wizara zinatakiwa kuendelea kuhamisha watumishi wake.

5. Septemba 2018 – Februari 2020.

Katika kipindi hiki, Wizara zinatakiwa kuendelea kuhamisha watumishi wake.

6. Machi 2020 – Juni 2020.

Katika kipindi hiki, Ofisi ya Rais ikiongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watakuwa wanahamia Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitumia wasaa huu kuzishauri Wizara zote kuanzisha mifumo ya utunzaji kumbukumbu wa kielektroniki badala ya kuhama na mafaili kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma, tunataka Dodoma iwe ya kielektroniki, alisisitiza Waziri Mkuu.

Alhamisi, 15 Septemba 2016

MAGAZETI YA TANZANIA SEPTEMBER 16, 2016 KUANZIA, UDAKU, HARDNEWS NA MICHEZO

.

September 16 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea mtu wangu.. usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook, twitter na instagram @millardayo ili niwe nakutumia kila kinachonifikia.
20160916_050558
20160916_050607
20160916_050616
20160916_050624
20160916_050633
20160916_050642
20160916_050650
20160916_050658
20160916_050708
20160916_050717
20160916_050726
20160916_050733
20160916_050756
20160916_050808
20160916_050816
20160916_050823
20160916_050833
20160916_050840
20160916_050848
20160916_050855
20160916_050903
20160916_050909
20160916_050917
20160916_050924
20160916_050938
20160916_050944
20160916_050954
20160916_051002
20160916_051010
20160916_051016
20160916_051031
20160916_051037
20160916_051111
20160916_051119
20160916_051141

20160916_051147
Source:millad ayo

FEYENOORD KAVUNJA REKODI YA MAN UNITED KATIKA HISTORIA


Bado mashabiki wa Man United wanashangazwa na maamuzi ya kocha Jose Mourinho kumuacha nahodha wao Wayne Rooney jijini Manchester na kusafiri hadi Uholanzi kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kundi A dhidi ya Feyenoord, huo ni mchezo ambao umechezwa katika dimba la Stadion Feijenoord.
3867052900000578-3791550-image-a-74_1473964112533
Kabla ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa Man United kuondoka vichwa chini kwa kukubali kipigo cha goli 1-0 lililofungwa na Tonny Vilhena dakika ya 79, takwimu ilikuwa inaonesha mara ya mwisho Novemba 5 1997 Man United alicheza katika uwanja huo na kuondoka na ushindi wa goli 3-1.
38668c6b00000578-0-image-a-37_1473960278617
Rekodi dhidi ya Feyenoord haikuisaidia Man United na badala yake wameondoka na huzuni kwa kuvunjwa rekodi yao ya kufungwa mechi nne za Europa League mfululizo ugenini katika historia , Man United sasa watashuka dimbani Septemba 29 Old Traffordkucheza dhidi ya Zorya ya Ukraine katika mchezo wao wa pili
.

DAKIKA 10 ZILIZOBADILI FURAHA YA KRC GENK YA SAMATTA EUROPA LEAGUE


Usiku wa Alhamisi ya Septemba 15 2016 ilikuwa siku ambayo macho ya watanzania wengi waliyaelekeza Australia kumuangalia nahodha wao wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta akiandika historia mpya katika maisha yake ya soka kwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ya Europa League akiwa naKRC Genk.
0025-1
Samatta ambaye alicheza kwa dakika 77 kabla ya kocha wake Peter Maes kumtoa na kumuingiza mgiriki Nokolaos Karelis, alitolewa wakati ambao timu yake ipo nyuma kwa goli 3-1 kabla ya dakika ya 90 mjamaica Leon Bailey kufunga goli la pili kwa mkwaju wa penati na kuufanya mchezo umalizike kwa sare ya goli 3-2.
67
Kipindi cha kwanza licha ya Genk kuzidiwa hali ya umiliki wa mpira kwa asilimia 53 kwa 47 walienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli moja lililofungwa na Leon Bailey ikiwa ni assist safi iliyotoka kwa Pozuelo alipewa mpira na Samatta, hali ilibadilika kuanzia dakika ya 51 hadi 60 Genk waliporuhusu kufungwa goli 3 ndani ya dakika 10.
Magoli ya Rapid Wien yalifungwa na Stefan Schwab dakika ya 51, Joelinton Cassiodakika ya 59 na nyota wa Genk aliyejifunga baada ya kumrudishia mpira kipa wakeMarco Bizot na kuukosa dakika ya 60, KRC Genk watacheza mchezo wao wa pili waEuropa League Septemba 29 wakiwa nyumbani dhidi ya klabu ya Sassuolo Calcio yaItalia.