Mwanamume
mmoja Raia wa Nigeria imebidi alazwe kwenye hospitali ya taifa ya
Kenyatta Nairobi Kenya baada ya kugundulika alikua na mzigo wa dawa za
kulevya wa vidonge 57 tumboni mwake.
Huyu jamaa alikua anazisafirisha hizi dawa kutoka Lagos kwenda
Bangkok lakini ghafla akaanza kupata maumivu baada ya kuchelewa
kufikisha mzigo aloubeba tumboni mwake baada ya ndege waliyokua
wakisafiria kutua Nairobi kwa dharura.
Ilitua kwa dharura baada ya rubani kuumwa ghafla hivyo kulazimu ndege
kutua Nairobi kisha abiria wote kupelekwa hotelini na hapo ndio
Mnigeria huyu akaanza kuhisi maumivu makali tumboni.
Simon
Ithae ambae ni mkuu wa mawasiliano hospitali ya Kenyatta amesema
‘alitueleza amemeza vidonge na alikua akiamini ndicho chanzo cha maumivu
hivyo alipoona hawezi kustahamili aliita Polisi akidai ameumizwa na
anahitaji kupelekwa hospitali lakini lengo lake ni apange njama na
madaktari kutoa dawa za kulevya bila yeye kukamatwa na aendelee nazo na
safari lakini mipango yake haikufanikiwa kwa sababu Madaktari walimpa
chakula ili kutoa dawa hizo na kisha wakawapa taarifa Polisi.
Alhamisi, 24 Julai 2014
Home »
» Mnigeria aliebeba dawa za kulevya alivyokamatwa Nairobi baada ya rubani kuugua.
0 comments:
Chapisha Maoni