Meriam Ibrahim akiwa na mumewe Daniel Wani pamoja na mtoto wao wa kwanza.
MWANAMKE wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kuasi dini ya Kiislamu na
kuolewa na Mkristo, Meriam Ibrahim, amesafirishwa kuelekea Italia baada
ya kukaa ubalozi wa Marekani mjini Khartoum, Sudan kwa zaidi ya mwezi
mmoja.
Meriam na familia yake wameondoka na ndege ya Serikali ya Italia
wakisindikizwa na Makamu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Lapo
Pistelli.
Awali Meriam alihukumiwa kifo na viboko 100 baada ya kuasi dini ya
baba yake ambaye ni Muislamu na kuolewa na Mkristo, Daniel Wani.
Baadaye mwanamke huyo alifanikiwa kuachiwa huru baada ya wanaharakati
kuingilia kati japo alikamatwa tena kabla ya kuachiwa na kukaa katika
ubalozi wa Marekani, Khartoum.
Alhamisi, 24 Julai 2014
Home »
» Binti wa SUDAN aliyehukumiwa kifo kwa kuasi dini ya UISLAMU ahamishiwa ITALIA
0 comments:
Chapisha Maoni