Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pope Francis Alhamisi ya July 24
2014 nchini Italia amekutana na Meriam mwanamke wa Sudan ambae
alihukumiwa kunyongwa nchini Sudan kwa kosa la kuolewa na mume Mkristo
mwaka 2011.
Meriam na watoto wake wawili akiwemo huyu wa mwisho aliezaliwa
gerezani pamoja na mume wake ambae ni raia wa Marekani mwenye asili ya
Sudan, waliwasili Italy wakiwa wameongozana na Afisa wa Italia ambae
alisaidia kwenye mazungumzo na serikali ya Sudan ambayo iliwashikilia
Meriam na mumewe kwa wiki kadhaa baada ya kuwakamata Airport wakiondoka
nchini humo.
Video iliyotolewa na Vatican imemuonyesha Pope akimpa Meriam medali
pamoja na rozari ambapo baada ya kukutana na Pope, wawili hawa wakiwa na
watoto wao watambatana kuelekea nchini Marekani ambako ndiko makazi yao
yalipo New Hampshire alikowahi kuishi mume wa Meriam.
Afisa wa Italia aliehusika kuongea na serikali ya Sudan ili familia
hii iachiwe, amesema ilibidi wawe wapole kwenye maongezi na ndicho
kilichosaidia mwishoni wakaachiwa huru baada ya kushikiliwa pamoja na
kwamba Mahakama kuu ya Sudan ilimuachia huru Meriam.
Meriam
mwenye umri wa miaka 27 alihukumiwa kifo baada ya kukataa amri ya
kurudi kwenye dini ya baba yake ambae ni Muislamu ambapo alifungwa
gerezani na kujifungulia mtoto wake wa pili hukohuko akiwa amefungwa
minyororo mpaka miguuni wakati wa kujifungua.
Alhamisi, 24 Julai 2014
Home »
» Mwanamke wa Sudan aliehukumiwa kifo kwa kuolewa na Mkristo amewasili Italia.
0 comments:
Chapisha Maoni