Liverpool
wapo tayari kumfuatilia tena Ryan Bertrand, 24, kutoka Chelsea, wakati
Brendan Rodgers akisaka beki wa kushoto (Daily Mail) kiungo wa Borussia
Dortmund Marco Reus, 25, na beki wa Southampton Dejan Lovren, 25, ni
miongoni mwa wachezaji Brendan Rodgers anawafuatilia (Daily Mirror)
Everton wanakaribia kumsajili Muhamed Besic, 21, kutoka Bosnia (Daily
Mirror), Tottenham wanafikiria kumtaka beki Ron Vlaar, 29, wa Aston
Villa, na wapo tayari kubadilishana na
Lewis Holtby au Michael Dawson (Daily Mail), Chelsea wanamfuatilia kwa
karibu beki Rafael Varane kutoka Real Madrid (Independent), Liverpool
wana matumaini ya kuuteka mchakato wa uhamisho wa kiungo wa Juventus
Arturo Vidal, 27, kwa kutoa dau la pauni milioni 42.5 walizotoa
Manchester United (Metro), meneja wa Everton Roberto Martinez
amethibitishwa kuwa anakaribia kumsajili David Henen, 18, kutoka
Anderlecht (Talksport), AC Milan wanamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal,
Joel Campbell, 22, na tayari wamewasiliana na klabu hiyo ya London
(Inside Futbol) Louis van Gaal anakabiliwa na mtihani mgumu baada ya
Borussia Dortmund kumuonya kuwa asahau kumsajili Mats Hummels, 25 (Daily
Express), Manchester United 'wameruhusiwa' kumsajili winga wa Real
Madrid Angel Di Maria, 26, baada ya timu hiyo kumsajili James Rodriguez
kutoka Monaco (Caughtoffside) hata hivyo taarifa nyingine zinasema Di
Maria anataka kwenda PSG kwa mkopo kwanza kabla ya uhamisho wa kudumu
msimu ujao (Daily Express), boss wa Chelsea Jose Mourinho amewaambia
makipa wake, Thiabaut Courtois, 22, na Petr Cech, 32, kuwa hawaendi
popote, watake wasitake (Times), Arsene Wenger yuko tayari kuacha
kutafuta kiungo mwingine, na atamuamini Jack Wilshere, 22 (Daily
Mirror), boss wa QPR, Harry Redknapp anataka kumsajili mshambuliaji wa
zamani wa Chelsea Samuel Eto'o (Daily Mirror) Romelu Lukaku wa Chelsea,
21, anakaribia kuondoka Darajani baada ya kufanya mazoezi na klabu yake
ya zamani Anderlecht (Sun). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Like na share kwa wingi hili kuongeza ushirikiano.
Alhamisi, 24 Julai 2014
Home »
» TETESI ZA SOKA ULAYA
TETESI ZA SOKA ULAYA
Related Posts:
Israel na Hamas waendelea na mapigano Mgogoro kati ya Israel na Palestina unaendelea. Pande zote mbili zimekuwa zikishambuliana kwa maroketi. Wakati huo huo, Misri inataka mazungumzo ya kuleta amani yaanze tena. Hali ya wasiwasi imerejea t… Read More
Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu ajali iliyotokea Tabora Aug 19. Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ambayo ameitoa leo kwa Waandishi wa habari ni kuhusu ajali ambayo ilitokea jana Aug 19 majira ya saa 9 alasiri ambayo ilihusisha mabasi mawili. Mabasi hayo ni AM Coach na S… Read More
RATIBA LIGI KUU BARA 2014/2015 HII HAPA Kocha … Read More
VIONGOZI WATUMIA MADARAKA YAO KUJINUFAISHA Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa … Read More
Waandamanaji wataka Nawaz Sharif ajiuzulu Waandamanaji wanopinga serikali nje ya bunge la Pakistan, hawaonyeshi ishara yoyote ya kuondoka,hadi pale waziri mkuu Nawaz Sharif atakapojiuzulu, dai ambalo serikali imekataa kwa misingi ya kuwai kinyume n… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni