Mama mzazi wa mkali wa bongofleva Nay wa Mitego ameongea kwa mara ya kwanza na millardayo.com na kusema ana wasiwasi na mwanae ambae hivi karibuni ametoa video mpya aliyoifanya nchini Kenya.
Amekiri kweli kwamba siku kadhaa zilizopita ilibidi amwite na kumuweka chini Nay wa Mitego akitaka amueleze kama ni kweli amejiunga na ‘freemason’ ambayo wengi wanaitafsiri kwamba ni dini ya kumwabudu shetani kitu ambacho kiliwahi kukanushwa na aliyewahi kuwa mmoja wa viongozi wa freemasons Tanzania.
Mama anasema alimketisha Nay chini baada ya video ya ‘Mr. Nay’ kutoka ambapo baadhi ya picha sio za kawaida mfano damu pamoja na alama zilizotumika ndani yake.
‘Nikiangalia miziki anayoifanya kama hii aliyoitoa juzi, jamani mwanangu anaambiwa freemason usikute kweli freemason, Nay wa Mitego nimemuita…. mwanangu vipi? ninayoambiwa ni ya kweli? Freemason wewe? mbona wimbo wako huu siuelewielewi? ananiambia mama mimi sio freemason, namwambia hapana mwanangu hapana….. nasikia freemason watu wanatoaga hata wazazi sadaka’
Unaweza kumsikiliza mama mzazi mwenyewe akiongea hapa chini…
0 comments:
Chapisha Maoni