Mshambuliaji mpya wa kilabu ya Arsenal Danny 
Welbeck anaweza kufunga mabao 25 kwa msimu mmoja ,hayo ni matamshi ya 
aliyekuwa mshambuliaji wa England Allan Shearer.
Wellbeck mwenye 
umri wa miaka 23 alijiunga na kikosi cha The Gunners kutoka kilabu ya 
Manchester United kwa kitita cha pauni millioni 16 katika siku ya mwisho
 ya dirisha la kuwasajili wachezaji wa soka barani ulaya na anaweza 
kuanzishwa kwa mara ya kwanza dhidi ya watetezi wa ligi hiyo Manchester 
City siku ya jumamosi.Nimesikia watu wakisema kwamba Wellbeck hawezi kufunga mabao 20 ama 25 kwa msimu mmoja ,sikubaliani na hilo Shearer aliiambia Radio 5 live ya BBC'',.
''Sasa ana uwezo wa kuonyesha umahiri wake katika ligi hiyo.''.
Siku ya Alhamisi Meneja wa kilabu ya Manchester United Van Gaal alisema kuwa Wellbeck hakuweza kufunga mabao ya kutosha wakati alipkuwa katika kilabu hiyo ya Old Trafford.
Mshambuliaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Manchester ambaye aliifunga mabao yote mawili timu ya Uingereza dhidi ya Switzerland siku ya jumatatu ,hajawahi kufunga zaidi ya mabao tisa katika ligi ya Uingereza tangu alipoanza kuchezea mwaka 2008.






 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni