Stori: Na Brighton Masalu
MAMBO yameiva!
Nyota wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ (20) yu
mbioni kupanda tena Kizimba cha Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es
Salaam kwa ishu yake ile ya madai ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa
msanii wa filamu nchini, marehemu , Amani lina ripoti mkononi.
Nyota wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa
chanzo chetu kutoka ndani ya mahakama hiyo jijini Dar, kesi hiyo
ilisimama kwa muda wa mwaka mmoja na zaidi kutokana na matatizo yaliyo
nje ya uwezo wa mahakama, lakini sasa matatizo hayo yameisha hivyo kesi
hiyo itaanza kurindima siku yoyote kuanzia sasa.
NI BAADA YA MWAKA MMOJA NA MIEZI NANE
Tangu kusimama
kwa kesi hiyo, mwaka 2013, ilitarajiwa kuanza tena kusikilizwa Februari
17, 2014 lakini ikakwama kutokana na matatizo mbalimbali ya kimahakama.
ITAANZA UPYA
Kwa mujibu wa
mtoa habari wetu, mwendesha mashtaka wa serikali atamsomea mashtaka upya
Lulu lakini neno la msingi kwenye mashtaka hayo ni; mnamo Aprili 7,
2012 anadaiwa kumuua bila kukusudia, Steven Kanumba.
“Baada ya
kuulizwa, Lulu akiwa kama Elizabeth Michael atajibu anachotaka kutoka
moyoni kulingana na ukweli anaoujua kisha jaji atampangia tarehe ya
kurudi tena,” alisema mtoa habari huyo.
MAHAKAMA ITATUMIA MWONGOZO WA JAJI MKUU
Tofauti na
madai ya awali kwamba, kesi hiyo ingeendeshwa kwa siku 730, habari za
uhakika zinasema kuwa, kesi itakapoanza safari hii haitasimamishwa mpaka
siku ya hukumu. Kwa hiyo itategemea na kasi ya hakimu husika.
“Lakini pia,
kauli ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman anayoitoa kila
Siku ya Sheria Duniani (Februari 3) kwamba kesi zote za jinai
zisipitishe miaka miwili, itazingatiwa,” kilisema chanzo.
Kikaongeza:
“Lakini nadhani ikianza safari mwaka huu, naamini mpaka mwaka 2017
itakuwa imemalizika kama sheria ya miaka miwili itazingatiwa.”
Marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ enzi za uhai wake.
CHENI BADO MDHAMINI
Chanzo hicho
kilisema kuwa, bado mcheza sinema maarufu Bongo, Mahsein Awadh ‘Dk.
Cheni’ anaendelea kutambulika na mahakama kama mdhamini wa Lulu. Kwa
hiyo, anatakiwa kuendelea na jukumu la kumlinda Lulu ili asiruke dhamana
(asitoroke, asikiuke masharti ya dhamana).
MASHAHIDI WAJIPANGE
Chanzo kilisema baadhi ya mashahidi muhimu nao watapewa taarifa ya kimaandishi ili tarahe ya kesi wafike mahakamani.
Mashahidi hao
ni Dokta Kidume ambaye alikuwa akimtibu Kanumba pia ndiye alikuwa mtu wa
pili kufika kwenye chumba cha marehemu mara baada ya kuanguka na
kupoteza maisha.
Seth Bosco
naye anatakiwa kujiandaa kupokea wito huo kwani yeye siku ya tukio
alikuwa nyumba moja na marehemu (vyumba tofauti). Yeye alimshuhudia
Kanumba akiwa katika hali mbaya baada ya kutoelewana na Lulu na kukimbia
kwenda kumwita Dokta Kidume.
WAKILI WA LULU AZUNGUMZA
Peter Kibatala ni wakili maarufu jijini Dar. Yeye ndiye mwanasheria katika kesi ya Lulu. Amani lilimtafuta ili kujua hatima ya kesi hiyo na madai kwamba iko njiani kuanza upya. Alisema:
“Aaa! Sijajua.
Lakini kwa kawaida mahakama itakapoona mambo yameanza, kesi inatakiwa
kuanza kusikilizwa itatakiwa kutoa taarifa siku sita kabla.”
AMZUNGUMZIA LULU
Wakili
Kibatala alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, mteja wake (Lulu)
amekuwa akimpigia simu mara kwa mara akitaka kujua tarehe ya kesi yake
kuanza tena.
“Hata Lulu
mwenyewe amekuwa akinipigia simu kuulizia ni tarehe ngapi kesi yake
itaanza tena. Nitapewa taarifa siku sita kabla,” alisema mwanasheria
huyo.
LULU PRESHA INAPANDA
Naye rafiki wa karibu wa Lulu, akizungumza na gazeti hili huku akiomba hifadhi ya jina lake, alisema:
“Ninyi
mnaandika Lulu siku hizi anakunywa sana pombe. Mnajua hayuko sawasawa.
Ile kesi yake ya kumuua (bila kukusudia) Kanumba inamtesa sana kichwani.
“Ukimya wa
kesi unamfanya ashindwe kujua hatima yake. Kila akikumbuka anampigia
simu wakili wake. Mbaya zaidi kuna watu wanamwambia kesi inaweza kukaa
kimya kwa muda mrefu halafu siku moja ikalipuka na kuwa nzito. Kwa hiyo
wakati mwingine mjue hilo.”
WASOMAJI WETU
Baadhi ya
wasomaji wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers wamekuwa wakipiga simu
chumba cha habari na kuulizia kama kesi ile ilifutwa kinyemela au
kihalali.
“Jamani
Global, mimi shida yangu ni kuulizia kuhusu ile kesi ya Lulu na Kanumba.
Hivi bado ipo au ilishafutwa kinyemela. Maana si mnajua watu maarufu
tena huenda kuna kubebana,” aliwahi kuuliza msomaji mmoja.
LULU ASAKWA
Jumatatu
na Jumanne iliyopita, simu ya Lulu ilipopigwa iliita muda mrefu bila
kupokelewa. Hata hivyo, baadhi ya watu wake wa karibu walisema Lulu huwa
hapokei simu ambayo jina halipo kwenye simu yake.
Source:GPL
0 comments:
Chapisha Maoni