CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachoungwa mkono na Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimetishia kutoshiriki katika Uchaguzi
Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi amesema wanadhamilia
kutoshiriki katika uchaguzi huo kutokana Tume yaTaifa ya Uchaguzi (NEC)
kutokuwa na msimamo katika kazi zake.
Anasema zikiwa zimebaki siku tatu wananchi kuelekea kwenye uchaguzi mkuu
lakini NEC hadi sasa haina msimamo na kuonekana kuyapuuza madai mengi
yenye hoja yanayotolewa na Ukawa.
Akiyataja baadhi ya madai ambayo NEC imeyapuuza ni kutotoa ushirikiano
wa kufafanua juu ya upigaji kura kwa watu ambao hawakuona majina yao
kwenye daftari la kupiga kura na kutotoa sababu ya utofauti wa namba za
kupigia kura kutoka kwenye daftari na kwenye kitambulisho.
Munisi ameongeza kuwa, NEC wamepuuza kutoa ufafanuzi juu ya picha ambazo
haziitajiki katika upigaji kura, kutoa ufafanuzi juu ya listi mpya ya
wapiga kura iliyosemwa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva,
kwamba kutakuwa na watu wa ziada ambao hawapo kwenye daftari, Je,
wanatoka wapi na wapo wangapi? Amehoji.
“Kwa mtindo huu ambao NEC inaenda nao wa kukubali watu wasiokuwa
kwenye daftari wapige kura na hata wasiokuwepo kwenye orodha wapige kura
mbona hawakutushirikisha sisi wadau wa uchaguzi? Inaweza kupelekea
uvunjifu wa amani. Hilo ndio bao la mkono ambalo lilisemwa na hatutaki
litokee,” anasema Munisi.
Munisi amesema sababu nyingine kubwa ambayo inaweza kupelekea
wasishiriki kwenye uchaguzi ni kuhusu madudu yaliyopo ndani ya daftari
la wapiga kura, ambapo hadi sasa NEC haijatoa jibu linaloeleweka juu ya
makosa ambayo yalionekana kwenye daftari.
Sababu nyingine ya kutaka kutoshiriki amesema, “Hatuna imani na
ujumlishaji wa matokeo ya kura kwa njia ya mashine zao za kujumlisha
kwani zinamapungufu mengi. Tuliomba tume itumie njia ya kawaida kwa njia
ya kalukuleta ili kila mtu alidhike lakini walidai tunawaingilia kazi
zake. Sisi hatutakubali,” amesema Munisi.
Kwa mujibu wa Munisi amesema, hadi sasa bado wanaendelea na uchunguzi
kwenye madaftari ya wapiga kura ambapo amesema wameshakagua katika mikoa
tisa na kubaini matatizo mengi zaidi yakiwemo ya picha hewa, picha za
watu wawili na majina ya kiume kwenye picha za kike.
“Hapo hatujafanya katika majimbo yote tulifanya baadhi. Bado
tunaendelea na uchunguzi hadi kesho, tukiona makosa yanazidi kiwango cha
kufanya uchaguzi usiende vizuri basi tunaiomba NEC ipeleke uchaguzi
mbele,” amesema Munisi.
Aidha, ameitaka NEC kutoa orodha maalumu ya vituo vya kupigia kura kwani
hadi sasa Ukawa bado hawajajua idadi kamili ya vituo hivyo wanashindwa
kuwaapisha mawakala kwa idadi ya vituo kubadilishwa kila siku.
Alhamisi, 22 Oktoba 2015
Home »
» UKAWA Watishia Kutoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Jumapili
UKAWA Watishia Kutoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Jumapili
Related Posts:
Zawadi kutoka kwa Barakah Da Prince – Sio Fine Kutoka Mwanza anaitwa Barakah Da Prince Mwanzoni ulimsikia na wimbo wa Jichunge ambao video yake ilifanywa na Director Nisher kutoka Arusha,leo July 02 ameamua kuachia wimbo wake ambao kasema ni zawadi maalum kwa mashabiki … Read More
Kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa mauaji ya Sista aliyepigwa risasi Ubungo. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam inawashikilia watuhumiwa wawili wa ujambazi ambao wanahusishwa na mauaji ya Mtawa wa Kanisa Katoliki Sista Clezensia Kapuli.Mbali na watuhumiwa hao pia watu wengine sita wanashi… Read More
Magazeti ya leo July 02 2014 … Read More
Taarifa kuhusu ndege iliyodondoka alfajiri ya July 02 Kenya. Imeripotiwa kuwa wanne waliokua kwenye Ndege iliyokua ikitokea uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Nairobi, Kenya kuelekea Mogadishu, Somalia wamepoteza maisha baada ya Ndege hiyo kuanguka katika eneo la Utawala dakika chache … Read More
Full time ya USA vs Belgium – walichofanya Lukaku na De Bruyne Mechi za hatua ya 16 zimemalizika rasmi usiku wa kuamkia leo kwa mchezo kati ya Marekani dhidi ya Belgium.Katika mchezo huo uliokuwa mgumu kwa pande zote, mpaka dakika zote 90 zinamalizika hakukuwa na mtu aliyefanikiwa kuli… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni