KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
amepata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea
jijini Dar es Salaam.
Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi alipata
ajali hiyo baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya
Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la
Nyangao mkoani Lindi.
Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha
gari hilo ambapo amepata majeraha madogo ila anaendelea vizuri.
Akizungumza na mtandao huu, Nape amesema: “Namshukuru Mungu nimetoka
salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya
maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na
michubuko ila ni mzima.
Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na ‘air bag’ nazo zimenisaidia.”
Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana
na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na
mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo
alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.
Source:GPL
Alhamisi, 22 Oktoba 2015
Home »
» Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye Apata Ajali Mbaya ya Gari
Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye Apata Ajali Mbaya ya Gari
Related Posts:
NICKSONLUV TECNOMILES waachia Ngoma yao inayofanya vizuri ulimwenguni play hapo chini kuona video &nbs… Read More
Jakaya Kikwete Aibukia 'Sauzi' Magufuli Akitumbua Majipu Magogoni Aliyomwachia.... Wakati Rais John Magufuli akitimiza siku 31 akiwa amejifungia Ikulu kutatua kero za nchi bila kusafiri nje ya nchi, Rais mstaafu Jakaya Kikwete (pichani) ameendelea kujumuika katika hafla za kimataifa baada… Read More
[Audio] Kauli ya Januari Makamba kuhusu kumkejeli Rais Magufuli January Makamba ameamua kutoa ufafanuzi wa picha mbalimbali zilizowekwa katika akaunti yake ya Instagram ambazo zinadaiwa kumkashfu Rais Magufuli baada ya kumnyima Uwaziri Mkuu. Hizi ndo Picha alizoweka amb… Read More
Tibaigana Afunguka...Huyu Ndiye Rais Niliyemtaka Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna mstaafu Alfred Tibaigana amesema Rais John Magufuli amepatikana wakati sahihi, kwa kuwa nchi inamhitaji kiongozi ambaye akitoa amri inatek… Read More
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Desemba 7, Ikiwemo ya Kukosekana Kwa Mawaziri Kwaokoa Mamilioni … Read More
0 comments:
Chapisha Maoni