Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema
nchi inahitaji rais mkali ili mambo yaende huku akishangazwa na mmoja wa
vigogo kufungua kesi kupinga mradi wa maji.
Amesema watu wa aina hiyo watakiona na anamuomba Mungu kwa siki tatu
zilizobaki apewe urais kwa vile hao ndiyo ataanza kushughulika nao.
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti katika
mikutano ya kampeni iliyofanyika Kigamboni, Mbagala, Temeke, Ubungo na
Kinondoni.
Alisema hayuko tayari kuona watu wanaendelea kupoteza maisha kwa kipindupindi huku kigogo huyo akikimbilia mahakamani.
Kitendo cha kigogo huyo kufunga njia ya maji kwa kujenga bomba la
majitaka kimesababisha wananchi wa Dar es Salaam kupoteza maisha kwa
kuugua kipindupindu, alisema.
“Ninajua hapa Temeke kuna mtu amekimbilia mahakamani na kukwamisha mradi wa maji lakini mahakama haitoi haki kwa wakati.
“Zimebaki siku nne ninichague kuwa rais, mtu anachelewesha mradi wa
maji kwa kwenda mahakamani ngoja nipate urais. Amejenga juu ya njia ya
maji watu wanakufa kwa kipindupindu haki ya Mungu ngoja nipate urais.
“…tunahitaji rais mkali mambo yaende kesi ni lazima iamuriwe kama
Serikali tumeshindwa tukate rufaa. Tena huyo mtu aliyefungua kesi ana
udugu na mmoja wa wagombea wa Ukawa,” alisema Dk. Magufuli.
Mgombea huyo wa urais alisema atakapochaguliwa Jumapili atakwenda kuanza na hilo.
“Haiwezekani, haiwezekani, haiwezekani mradi wa maji una manufaa wao
wanakunywa maji ya Kilimanjaro wananchi wanateseka. Lakini watu wachache
kwa tamaa zao na madaraka yao wanakwamisha.
“Wanasema mimi ni mkali, hapana nina hofu ya Mungu, tunaomba kesi hii iamuriwe kama tumeshindwa tukate rufaa,” alisema Dk. Magufuli
Mgombea huyo wa urais alisema yeye ni mtu wa uamuzi makini anayekuja
kuijenga Tanzania mpya na yenye matumaini kwa watanzania wote.
Alisema anashangazwa na watu wanaohangaika na uamuzi mgumu kwani wanaofanya hivyo ni majambazi, wezi na mafisadi pekee.
Dk. Magufuli, alisema ataongoza taifa kwa umakini kwa kuleta maendeleo ya kweli.
Alisema anashangazwa na watu wanaopita na kujinasibu kwa kuleta uamuzi
mgumu wakati ndiyo walioleta matatizo katika nchi na hata kusababisha
kero ya umeme kila kukicha.
“Watakuja wapinzani wetu na kusema eti wanakuja na uamuzi mgumu,
jamani uamuzi mgumu hufanywa na majambazi, wezi na wauaji wa watu wenye
albino. Inashangaza sana hawa watu msiwakubalie hata kidogo.
“… hivi jana itokee upate mume au mke anayetamba kwa kuwa na uamuzi
mgumu si atakunyonga kitandani. Eti atafanya uamuzi mgumu mbona
hujinyongi kwa kamba? Mimi kwangu Magufuli kazi tu,” alisema Dk. Magufuli.
Akizungumzia ujenzi wa daraja la Kigamboni, Dk. Magufuli alisema
litakamilika mwezi ujao na wananchi wa eneo hilo watavuka bure ila watu
wenye magari ndiyo watakaolipa ada.
Alisema yeye ni mtu anayesimamia sheria hivyo katu hawezi kuzivunja
kwa kutoa ahadi za uongo kwa lengo la kutafuta kura za watanzania.
“Daraja la Kigamboni litakamilika mapema mwezi ujao na litakapokamilika
wakazi wa Kigamboni watapita bure ila wenye magari watalipia kama
ilivyokuwa kwenye kivuko cha pantoni.
“Kigamboni ya sasa imekuwa na maendeleo na kwa sababu mbunge wenu,
Dk. Ndugulile (Faustine) ni mfuatiliaji nami nawaomba mumchague
ninamuhitaji.
“Alipambana kwa ajili ya yenu na sasa ninasema hapa Rais Jakaya
Kikwete amenisaidia sana kwa kuiteua Kigamboni kuwa wilaya nami kazi
yangu itakuwa ni kuleta maendeleo ya kweli,” alisema.
Mgombea huyo wa urais alisema kwa mujibu wa sheria, ardhi ni mali hivyo
kwa Kigamboni kujengwa mji mpya ni hatua kubwa ya maendeleo.
Dk. Magufuli aliwataka wakazi hao kuhakikisha wanasimamia haki zao
ikiwamo kumiliki ardhi yao na hata kushirikiana na wawekezaji.
“Ardhi ni mali na hapa Kigamboni sasa mji mpya wakija wawekezaji
kwanza wawape noti na hata mshirikiane pamoja kutokana na ardhi yenu,” alisema.
Chadema wampokea Ubungo huku wakimshangilia Lowassa
Mgombea huyo wa urais wa CCM alipofika katika Kituo cha Mabasi Ubungo,
alisimamishwa na wafuasi wa Ukawa ambao walimnyoonshea vidole viwili
juu huku wakimshangilia Mgombea wao kwa kuimba Lowassa!!!
Lowassa!!
Baada ya hali hiyo,Magufuli aliwasalimia wafuasi hao wa Ukawa
kwa ishara ya salamu zao na kuwaambia kuwa maendeleo hayana
chama.
“Maendeleo hayana chama iwe Chadema, CCM, CUF na hata Ukawa mimi kwangu ni kazi tu,” alisema.....Tazama Video Hii
https://youtu.be/NI_JKb9KJSc
Alhamisi, 22 Oktoba 2015
Home »
» Magufuli Asimamisha Jiji La Dar.......Asema Tanzania Inahitaji Rais Mkali. CHADEMA Wampokea Kwa Ishara Ya Vidole Viwili Juu
Magufuli Asimamisha Jiji La Dar.......Asema Tanzania Inahitaji Rais Mkali. CHADEMA Wampokea Kwa Ishara Ya Vidole Viwili Juu
Related Posts:
Wasafi Wadaiwa Kumpora Producer Frag Ngoma ya 'Bado' iliyoibwa na Harmonize Feat. Diamond Producer Frag kutoka Uptown Music ametumbua jipu baada ya kuibuka na kusema kuwa yeye ndiye aliyetengeneza wimbo wa Bado wa Harmonize na Diamond. Frag aliiambia Enewz kuwa pamoja na kazi kubwa aliyoifanya kuhakikisha ngoma… Read More
VYAKULA VINAVYO ONGEZA HISIA KATIKA MAPENZI Kama kawaida mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho kutoka au kamasi. Kwenye pilipili kuna kitu kinaitwa Capsaicin ambacho hufanya pilipili i… Read More
ITALIA WAJA NA UTAALAMU WA KUPANDIKIZA KICHWA KWA MTU Mtaalam wa upasuaji wa mfumo wa neva (neurosurgeon) Sergio Canavero kutoka nchini Italia, anakusudia kufanya jaribio la kwanza la kupandikiza kichwa cha binadamu kwenye mwili wa binadamu mwingine, ifikapo mwakani. Wataalam… Read More
Siri Kuu Kuhusu Escrow zafichuka SIRI kuu ya James Rugemalira, kumwaga mabilioni ya shilingi kwa baadhi ya majaji wa mahakama kuu, viongozi waandamizi serikalini na madhehebu ya kidini, wabunge na viogogo wa Ikulu, zimeanza kufumuka. Nyaraka mikononi mwa ga… Read More
Punguzo Kodi ya Mishahara Kwa Wafanya Kazi Laibua Mapya Uamuzi wa Rais John Magufuli kupunguza asilimia mbili ya Kodi ya Mshahara (PAYE) umeibua mjadala baada ya kubainika kuwa utampa nafuu ndogo mfanyakazi, huku wachambuzi wakihamia kwenye kodi nyingine ya mapato kwa kuzingatia … Read More
0 comments:
Chapisha Maoni