Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi (kulia) akifafanua
jambo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Prof. Abdallah
Safari
**
ZIKIWA zimebaki siku tatu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka
huu, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefichua mikakati
iliyopangwa kuvuruga uchaguzi huo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi amebainisha mipango
‘ovu’ inayoratibiwa ili kuvuruga uchaguzi mkuu huku mipango hii
ikishirikisha baadhi ya makampuni ya simu za mkononi, Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) na wakurugenzi wa uchaguzi katika majimbo mbalimbali.
Munisi ametaja baadhi ya mipango hiyo kama ifuatavyo, huku
akitahadharisha watakaoshiriki mipango hiyo kuwa wataliingiza taifa
katika machafuko bila sababu ya msingi.
Mpango wa kukata mawasiliano ya simu na data; upo mpango wa kuzuia
mawasiliano ya simu za mkononi kwa kusitisha huduma ya kupiga na kupokea
simu, kuzuia ujumbe mfupi wa maneno (sms), kuzuiwa kwa intaneti (data)
na hivyo mawasiliano kuwa magumu, hasa wakati wa matokeo kubandikwa
vituoni.
Mpango huu unatajwa kuwa na lengo la kukwamisha watu kuwasiliana na
kupeana matokeo yatakayokuwa yakibandikwa vituoni ili kujumlisha na
kupata matokeo ya jumla ya nafasi za udiwani, ubunge na urais.
Utekelezaji wa mpango huu utashirikisha baadhi ya makampuni ya simu
ambayo hakutaka kuyataja.
“Tunaziomba kampuni za simu zenye mpango huo, kuacha mara moja kwani
zitajiongeza katika orodha ya watuhumiwa watakaoenda ‘The Hague’ mara
baada ya uchaguzi kumalizika,” alieleza Munisi bila kuyataja makampuni
hayo kwa kuwa bado chama hicho kinakusanya vielelezo.
Mpango wa kukata umeme maeneo yenye nguvu kubwa ya upinzani; maeneo
ambayo vyama vya upinzani vina nguvu kubwa umeme utakatwa baada ya giza
kuingia ili kuhakikisha mchakato wa kuhesabu na kujumlisha matokeo
unaingia dosari na hata vurugu kutokea ili katika taharuki hiyo wizi wa
kura uweze kufanyika.
Baadhi ya wakurugenzi wa uchaguzi kutoruhusu mawakala wa akiba wa
upinzani kuapishwa; wakati uapishaji wa mawakala ukiendelea katika
maeneo mbalimbali nchini, baadhi ya maeneo vyama vya upinzani vinazuiwa
kuapisha mawakala wa akiba na wakurugenzi kutaka mawakala waape idadi
sawa na idadi ya vituo vya kupigia kura.
Mkakati huu unalenga kuvifanya vyama vya upinzani vikose mawakala wa
akiba iwapo itatokea dharura miongoni mwa wale walioapishwa, dharura
zinazoweza kujitokeza ni kuumwa, kusafiri nje ya vituo, au kutekwa kabla
ya kufika katika vituo vyao.
Iwapo mawakala hao watakosekana kwa dharura, baadhi ya vituo watabaki
mawakala wa CCM pekee kwani hakutakuwa na mawakala wa akiba wa kuziba
nafasi zao kwa kuwa ni lazima mawakala wawe wamekula viapo vya kisheria
ili kupata uhalali wa kufanya kazi hiyo.
Reginald Munisi ameleza kuwa Chadema na Ukawa kiujumla wamejipanga vyema
kuzikabili mbinu hizo chafu huku akiwaonya wale watakaoshiriki mipango
hiyo kuachana nayo mara moja kwani tayari imefahamika na wanaweza
kukumbana na nguvu ya Umma.
Alhamisi, 22 Oktoba 2015
Home »
» CHADEMA Wafichua Mbinu Zilizopangwa Kuvuruga Uchaguzi wa Jumapili hi
CHADEMA Wafichua Mbinu Zilizopangwa Kuvuruga Uchaguzi wa Jumapili hi
Related Posts:
Jinsi Beyonce alivyobadilisha mistari ya wimbo wake jukwaani kufuatia matatizo ya ndoa yake. Wanandoa Beyonce na Jay Z wamekuwa wakipambana na uvumi kuwa sasa ndoa yao iko juu ya mawe kutokana na matatizo makubwa yanayoendelea tangu kusambaa kwa video ikimuonyesha dada wa Beyonce Solange akimshambulia Jay Z. Na s… Read More
Angalia magoli 10 bora ya kombe la dunia – Messi vs Van Persie nani katisha? Michuano ya kombe la dunia ipo kwenye hatua ya robo fainali ambayo itaanza rasmi Ijumaa hii. Michuano hii ya mwaka huu imekuwa na magoli mengi na bora katika historia ya michuano hii mikubwa kabisa katika soka.youngluvega.c… Read More
Taarifa ya Kaimu Balozi wa Libya, Tanzania aliyejiua kwa kujipiga risasi. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania leo imepokea taarifa kutoka ubalozi wa Libya nchini ikieleza kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya Bw. Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risa… Read More
Dar es salaam Julai 02, 2014, Gari hili la Magereza lapigwa risasi likiwa na wafungwa ndani. Taarifa za awali zinadai kuwa Basi lililokuwa limebeba wafungwa limeshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana eneo la Mayfair Mikocheni jijini Dar es salaam.Basi hili lilikuwa likitokea mahakama ya Mwanzo Kawe ambapo kwa… Read More
Malalamiko ya Shilole kuhusu Dj wa Club anayetaka kumdhulumu Laptop yake. Kutoka kwa Soudy Brown kupitia You heard ya leo Shilole amelalamika juu ya mtu anayedai kumuazima laptop yake lakini anaonekana ana dalili za kumdhulumu baada ya simu zake kuwa hapokei, amemtaja kwa jina la Dj Ommy Crazy am… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni