Uongozi wa Uchumi Supermarket umetangaza kufunga shughuli zake katika
maduka yake yaliyopo Tanzania na Uganda ili kutoa nafasi ya kuzuia
mtikisiko wa kifedha unaoikumba kampuni hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk Julius Kipng'etich, amesema Bodi
imeamua kufunga vitengo vya kikanda ili kuimarisha shughuli zake nchini
Kenya baada ya kupata hasara katika maduka yake ya Uganda na Tanzania.
"Maduka yetu ya Uganda na Tanzania huchangia asilimia 25 tu ya gharama
za uendeshaji. Matawi hayo mawili hayajapata faida yoyote kwa zaidi ya
miaka mitano iliyopita jambo linaloyumbisha shughuli zetu," amesema Dk
Julius
"Tuna uhakika kwamba tunaweza kuigeuza Uchumi kwa kulenga asilimia 95 ya
biashara ambazo zinaleta fedha kwa wanahisa ambao wana matumaini kwamba
tutafanikisha hili ndani ya muda mfupi," ameongeza Dk Kipng'etich.
Kwa upande wa Tanzania, juzi wafanyakazi zaidi ya 400 waligoma kwa
kujifungia ndani ya ofisi zao kwa zaidi ya saa 20 wakitaka kujua hatma
yao kwenye makao makuu ya duka hilo yaliyopo katika jengo la Quality
Center jijini Dar es salaam.
Alhamisi, 15 Oktoba 2015
Home »
» MADUKA YA UCHUMI SUPERMARKET YAFUNGWA TANZANIA NA UGANDA
MADUKA YA UCHUMI SUPERMARKET YAFUNGWA TANZANIA NA UGANDA
Related Posts:
New AUDIO | TMB FT GENTRIEZ - NIPO MBALI NA HOME | Download … Read More
New AUDIO | SNAIDA - MUHTASARI WA HABARI | Download ARTIST-SNAIDA. SONG-MUHTASARI WA HABARI. STUDIO-BANTU MUSIC. PRODUCED BY LUSUNGU https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYh_iqvVbGTqdX8O2R6FpqP8Jot3LTk6a5V2ValJu2sODDSoid6ivcGTcb5_JN64qKkLvdij2JD721xHB… Read More
VIDEO | SAMIR - FITINA | watch&Download … Read More
VIDEO | Sitiky ft Kijo - Maisha Yake | watch&Download … Read More
Sikiliza hapa ugomzi uliotokea dakika 5 kabla ya Show ya XXL Clouds Fm kumalizika Julai 02 Kilichosababisha haya yote ni mabishano ya mauzo ya album ya Fiesta ambayo kila mmoja alikua anataka aiandae alafu aiuze yeye….. ilitokea B12 alisema ni wazo lake lakini kumbe Fetty na Adam nao wanasema waliwahi kuwa na waz… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni