BIASHARA imekwisha! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia ‘kapo’ ya staa wa 
Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The
 Boss Lady’ kudaiwa kuwa waliweka misingi ya penzi zito ili Diamond 
apate mtoto hivyo baada ya mrembo huyo kujifungua Latifah ‘Tiffah’ miezi
 miwili iliyopita, penzi halitakuwa motomoto kama zamani, Risasi 
Jumamosi lina ‘full’ stori.
Chanzo cha uhakika kilicho karibu na wawili hao, kimesema makubaliano ya
 awali baina ya wazazi hao, yalikuwa ni kwa mwanamke huyo raia wa 
Uganda, kumzalia mtoto Diamond ambaye alikuwa akisaka ubaba kwa udi na 
uvumba.
TUJIUNGE NA CHANZO
“Wote mnajua jinsi Diamond alivyokuwa akihangaika kupata mtoto, maana 
wapenzi wake wote wa awali hawakuweza kumzalia. Sasa alipokutana na Zari
 ambaye tayari alikuwa na watoto, wakakubaliana kwa masharti kuwa ndani 
ya muda f’lani, amzalie.
“Sasa ndiyo ikawa hivyo, baada ya Tiffah kuzaliwa, kila mtu sasa yupo 
huru kufanya yake, ndiyo maana Zari amerudi kwake Afrika Kusini ‘Sauz’ 
na hawezi kuja kuendelea kuishi na Diamond kama wakati ule wa ujauzito.
“Kule Sauz, Zari anaendelea na biashara zake na nimesikia kwa sasa 
anaandaa Zari All White Party kama ile aliyoifanya Mlimani City hapa 
Bongo,” kilisema chanzo chetu.
Msanii chipukizi wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WBC’ aitwaye Harmonizer akilishwa keki na Rose.
KWA NINI HAWEZI KURUDI?
Chanzo hicho kiliendelea kutoboa siri kwamba, pamoja na makubaliano ya 
kuzaa, lakini pia mazingira ya sasa ya makazi ya Diamond hayatoi nafasi 
kwa mwanamke huyo mwenye fedha ambaye pia ni msanii, kuweza kuishi.
“Sasa hivi pale nyumbani kwa Diamond kumejaa, imekuwa familia kubwa. 
Maana kuna mjomba wake Diamond anaishi pale, dada zake wawili, Esma na 
Queen Darleen wanaishi pale. Mama yake Diamond (Sanura Kasim) yupo pale.
“Haya, achana na ndugu wengine. Lakini pia kuna wasichana wa kazi wawili
 na mlinzi mmoja. Sasa kwa mtu kama Zari ambaye maisha yake ni ya 
kisupastaa hawezi kuishi kwenye nyumba yenye watu wengi hivyo.”
ZARI ANAOGOPA UMBEYA
“Pia inasemekana Zari hataki kuishi na wifi zake kwa sababu anaogopa 
umbeya. Hata wakati ule alipokuwa mjamzito mpaka kujifungua, hakuwa mtu 
wa kujichanganya nao sana. Alikuwa mtu wa peke yake peke yake tu.”
HAKUNA TENA MAPENZI?
“Taarifa nilizonazo ni kuwa, Diamond na Zari watakuwa wanaendelea na 
uhusiano wao wa kimapenzi lakini si ule wa kama awali. Ila wataendelea 
kuwa watu waliozaa mtoto na maisha ya Tiffah yataendelea kuwa kwa mama 
yake hadi hapo watakapoamua vinginevyo. Zari anaweza kuja Bongo na 
Diamond anaweza kwenda Sauz kwa Zari.”
“Zari hataki kuishi Tanzania, anataka Tiffah aishi na ndugu zake kule 
Sauz hadi akue na kuanza masomo. Kwa hiyo usitegemee ule ukaribu kama wa
 mwanzo.”
KUHUSU DIAMOND!
Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia suala hilo ziligonga 
mwamba ikielezwa kuwa yupo nchini Marekani katika shughuli za kimuziki. 
Hata alipotumiwa meseji kwa njia ya Mtandao wa WhatsApp hakujibu.
Hata hivyo, mtu wake wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alitatizwa na suala hili akisema:
“Dah! Wabongo bwana! Ninachojua mimi ni kuwa, bado watakuwa wapenzi 
japokuwa siwasemei maana Diamond naye haaminiki sana. Si unajua 
ameshapata mtoto, lolote linaweza kutokea.
“Ila Diamond akimhitaji Zari aje Tanzania anaweza kuja, akitaka aende 
Sauz atakwenda kwa sababu Tiffah lazima alelewe na wazazi wote.
“Halafu lazima ujue kwamba, Zari ni mfanyabiashara, ana biashara zake 
Afrika Kusini na Uganda. Kwa hiyo siyo mtu ambaye unaweza kumtegemea 
akae sehemu moja tu.”
Alhamisi, 15 Oktoba 2015
Home »
 » ZARI NA DAIMOND ETI BASI TENA..BIASHARA KWISHNEY







0 comments:
Chapisha Maoni