Alhamisi, 15 Oktoba 2015

MGOMBEA WA URAISI CCM DR. JOHN POMBE MAGUFULI AMFAGILIA DAIMOND PLATNUMZ

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli amemmwagia sifa lukuki, mkali wao ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutokana na ushindi wa tuzo tatu za Afrimma zilizofanyika wikiendi iliyopita nchini Marekani
Tukio hili lilitokea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mpilipili mkoani Lindi baada ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba kushuka jukwaani kukamua kwenye kampeni za mgombea huyo wa urais, ndipo Magufuli alishika kipaza sauti na kumsifia Diamond aliyeshinda tuzo za Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki, Msanii Bora wa Mwaka na Utumbuizaji Bora wa Video.

“Ukweli nampongeza sana msanii Diamond kwa jinsi anavyojituma na kuipeperusha vyema bendera ya taifa letu…,” alisema Magufuli huku pia akiwapongeza Ommy Dimpoz na Vanesa Mdee walioshinda tuzo tofauti katika kinyang’anyiro hicho.

Aidha, katika kampeni hizo Magufuli aliwaahidi wakazi wa mji huo kuwajengea Lindi mpya ambayo itakuwa ya neema kupitia gesi inayopatikana kwenye ukanda huo, unafuu wa vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji ‘cement’ iliyoanza kupatikana kwa bei ya shilingi 8,000 kwenye kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara, zao la korosho ambalo Magufuli alijinandi kuwa na digrii ya zao hilo.

Related Posts:

  • Waaga mchuano baada ya kuagizwa kuvua hijab Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa kikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia. Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa vikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia yanayofanyika huko Korea Kus… Read More
  • Taarifa kuhusu kifo cha msanii wa bongofleva Side Boy Mnyamwezi. Ingawa Nafasi yake katika muziki wa Bongo Fleva ilikuwa ikipanda taratibu kulingana na aina ya muziki aliokuwa akiumba,single iliyomtambulisha zaidi kwenye muziki wa Bongo Fleva inaitwa Kua uone ambayo alimshirikisha A… Read More
  • NI KIVUMBI LIGI YA MABINGWA ULAYA   Katika michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya leo kuna kivumbi kingine ambapo CSKA Moscow itakuwa na kibarua kigumu pale watakapowakaribisha Bayern Munich. Wakati huo huo Man City waliopigwa bao moja na Bayer… Read More
  • 'VIPIMO VYA SKETI KIGEZO CHA SARATANI'  Baadhi ya watafiti wana sahuku ikiwa vipimo vya sketi vitamtahadharisha mwanamke kuhusu tisho la Saratani. Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanaonenepa maishani bila ya kuwa waangalifu wanajiweka katika hatari ya kupa… Read More
  • Van Gaal:tuna mlinzi wa kati mmoja tu  Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal. Kocha wa machester United, Louis van Gaal amesema Manchester united ina mlinzi wa kati mmoja tu mwenye uzoefu wakati huu kikosi hicho kinapotarajia kukipiga na west ham kat… Read More

0 comments:

Chapisha Maoni