Rais Jakaya Kikwete amesema watu wanaopanga kubaki katika vituo vya
kupigia kura baada ya kumaliza zoezi hilo kwa lengo la kulinda kura
kunaashiria uvunjaji amani, hivyo serikali imejipanga kupambana na hali
hiyo siku ya uchaguzi.
Rais amesisitiza kwamba wanaopaswa kulinda kura ni mawakala pekee na si wafuasi wa mgombea ama vyama.
Akizungumza jana katika sherehe za Kilele cha Mwenge wa Uhuru
zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kiongozi huyo anayemalizia
muda wake madarakani alisema viongozi wanaowaagiza wafuasi wao kulinda
kura wana nia mbaya dhidi ya amani ya nchi.
“Mnatakiwa muondoke kwenye vituo baada ya kupiga kura….kura
utazilindaje? Mawakala ndio pekee wanaoweza kulinda. Mkikaidi hilo,
hatutawavulimia. Serikali imejipanga kupambana na wale wote watakaokaidi
agizo la Tume ya Uchaguzi (NEC),” alisisitiza Rais Jakaya Kikwete.
Katika shehere hizo za mwenge zilizoendana sambamba na maadhimisho ya
siku ya kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete
aliwataka Watanzania kuchagua watu waadilifu ambao wana dhamira ya
kupambana na rushwa kwa vitendo.
“Tumchague mtu ambaye hana ukabila, udini na ubaguzi wa rangi…tumchague
kiongozi atakayetetea maslahi ya makabila yote 126,” alisema rais huku
akimnukuu Mwalimu Nyerere aliyefariki miaka 16 iliyopita.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa pia na Spika wa Bunge anayemaliza muda wake,
Anne Makinda, wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa ngazi tofauti
serikalini na kupambwa na nyimbo za makabila na wanafunzi wa shule
mbalimbali mjini Dodoma.
Alhamisi, 15 Oktoba 2015
Home »
» RAISI KIKWETE AWAONYA WANAOPANGA KULINDA KURA VITUONI
RAISI KIKWETE AWAONYA WANAOPANGA KULINDA KURA VITUONI
Related Posts:
Habari njema! Fastjet tena kwenye headlines!! wameanza kwenda Uganda. Shirika la ndege la Fastjet limepata sifa kubwa nchini Tanzania kutokana na kusafirisha kwake abiria na kuanza kuiunganisha Afrika kwa kasi ambapo baada ya kuanzisha safari za nyumbani kati ya Mwanza – Dar, Kilimanjaro – D… Read More
UGANDA YAHARIBU SHAMBULIZI LA KIGAIDI Vikosi vya usalama nchini Uganda Maafisa wa polisi nchini Uganda wameimarisha usalama katika maeneo mengi ya uma katika mji mkuu wa Kampala kufuatia kukamatwa kwa washukiwa kadhaa wa makundi ya kigaidi na vil… Read More
WANACHAMA 100 WA BOKO HARAM WAUAWA jeshi la Nigeria Jeshi la Nigeria linasema kuwa limewaua zaidi ya wanamgambo 100 wa kundi la Boko Haram kufuatia shambulizi la wapiganaji hao siku ya ijumaa kazkazini mashariki mwa jimbo la Borno. Vikosi vya ser… Read More
MAYWEATHER AMCHAPA TENA MAIDANA Floyd Mayweather (kushoto) akimtupia konde mpinzani wake Marcos Maidana. Maidana akijibu mashambulizi wakati wa pambano hilo. Mayweather akimshambulia mpinzani wake.… Read More
MFUNGWA AKUTWA NA SIMU MWILINI Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ya Kenya imekuwa kero kubwa kwa maafisa wa magereza. Kwa baadhi ya watu simu ya mkononi ni kifaa tu cha mawasIliano ilihali kwa wengine ni kifa ambacho kinaweza … Read More
0 comments:
Chapisha Maoni