Serena Hotel |
HOTELI
ya kimataifa ya Serena jana ilikumbwa na msukosuko wa kuandamwa na
waandishi wa habari baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa imefungwa kwa amri
ya serikali kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.
Tetesi
hizo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jana asubuhi,
zikieleza kuwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wameifunga hoteli
kufunga kwa kukwepa kuliko kodi serikalini.
Mbali
ya kusambazwa kwa uvumi huo, zilitumwa pia picha zilizokuwa zikionyesha
sehemu ya hoteli hiyo ikiwa imezungushwa uzio uliokuwa na rangi nyeupe
na nyekundu ambao ni alama inayotumika kuonyesha kusitisha kwa huduma
katika eneo hilo.
Tetesi
hizo zilikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa uongozi wa hoteli hiyo
ulikuwa mbioni kubadilisha jina kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.
Hata
hivyo, mwandishi wetu baada ya kufika hotelini hapo kwa lengo la
kufuatilia ukweli wa tetesi hizo alikuta shughuli za ukarabati wa sehemu
ya kupokea wageni zikiendelea, huku wageni wakielekezwa kutumia mlango
wa dharura ambako kumetengezwa sehemu ya muda ya kupokelea wageni.
Uongozi
wa Hoteli ya Serena kupitia Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko, Seraphine
Lusala, ulilazimika kutoa taarifa kwa vyombo vya habari ukikanusha
kufungwa kwa hoteli hiyo na kusisitiza kuwa kinachoendelea hotelini hapo
ni matengenezo.
“Si
kweli kama hoteli imefungwa, tunafanya matengenezo na yalikuwa
yafanyike tangu miaka mitatu iliyopita, kilichofanyika sasa ni
kubadilisha eneo la mapokezi yaliyohamishiwa milango mingine na tumeanza
na eneo hilo pamoja na sehemu ya mazoezi,” alisema Lusala.
Alisema matengenezo hayo yanalenga kuifanya hoteli hiyo kuwa ya kiwango cha juu zaidi na yatachukua miezi 10.
Lusala
alisema awamu ya kwanza ya matengenezo itachukua miezi minne na miezi
minne ijayo itahusu matengenezo sehemu ya vinywaji, chakula, eneo la
uwanja na baadaye maeneo mengine ya wazi.
0 comments:
Chapisha Maoni