WAKATI
Rais John Magufuli akiwa kwenye zoezi la kutumbua majipu kwenye Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), mshtuko
mkubwa umetokea kufuatia kigogo mwenye wadhifa wa Artsan One (TPA)
jijini Dar, Elia Eliampenda Kimaro (51) kufariki dunia ghafla kwa
shinikizo la damu (presha) akiwa nyumbani kwake, Mikwambe, Kigamboni,
Dar.
Kimaro
alifariki dunia Novemba 30, mwaka huu kwa uthibitisho wa daktari wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako marehemu alikimbizwa kwa ajili
ya matibabu.
Kifo
cha Kimaro kimetokea wakati kukiwa na sintofahamu kubwa miongoni mwa
wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuhusiana na utolewaji wa makontena 349
kinyemela na kuisababishia serikali kukosa mapato ya kiasi cha shilingi
bilioni 80.
Taarifa
kutoka ndani ya familia, marehemu alisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda
mrefu. Lakini ghafla alfajiri ya Novemba 30, hali yake ilibadilika na
hivyo kukimbizwa Muhimbili ambako daktari alisema alishafariki dunia.
Mwandishi
aliweza kufika msibani ambapo aliwashuhudia wafanyakazi wengi wa
bandarini na TRA bandarini wakiwa hapo kwa ajili ya maandalizi ya
mazishi.
Baadhi
ya wafanyakazi hao, walisikika wakidai, marehemu alikuwa miongoni mwa
vigogo waliokuwa wakichunguzwa kwa utolewaji wa makontena 349 siku
chache zilizopita.
“Pia
nasikia baada ya waziri mkuu (Kassim Majaliwa) kutoa mwongozo siku zile
bandarini, watu wa usalama wa taifa walishamfuata hapa kwake mara
kadhaa na kumhoji.
"Lakini
pia, kuna madai kwamba, miamala yake ya kibenki nayo ilifuatiliwa na
jamaa hao ambapo walikuta pesa nyingi,” alisikika akisema mmoja wa
wafanyakazi hao ambaye alipogundua kuna waandishi wa habar alifunga
kinywa.
Nao
baadhi ya waendesha bodaboda wa eneo hilo, walionekana kushangazwa sana
kufuatia taarifa za kifo cha kigogo huyo, wakidai siku moja kabla,
walionana naye akiwa mzima wa afya.
Hata
hivyo, walisema mara baada ya taarifa za kifo, walishangaa kuona magari
yake ya kifahari yakiondolewa kutoka nyumbani kwake hapo:
“Labda
waliyapeleka mahali ili kupata nafasi ya kuweka maturubai ya msiba. Si
unajua majumba haya ya ghorofa, yana nafasi zaidi ya kwenda juu kuliko
upana,” alisema mmoja wa bodaboda hao.
Mwendesha
bodaboda mmoja alisema: “Mzee wa bandari alikuwa mtu poa sana. Hata
madereva wa daladala zake wameumia. Unajua jamaa alikuwa na mkwanja wa
maana. Hii nyumba ya hapa ‘cha mtoto’, ana nyumba nyingine Yombo (Dar),
magari ndiyo usiseme. Yaani tumempoteza mtu muhimu sana.”
Marehemu Kimaro alizikwa Desemba 2, mwaka huu kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar. Ameacha mke na watoto wanne.
Credit: GPL
Jumamosi, 5 Desemba 2015
Home »
» Kigogo wa Bandari Afariki Kwa Presha...Undani wa Kifo chake Waelezwa Hapa
Kigogo wa Bandari Afariki Kwa Presha...Undani wa Kifo chake Waelezwa Hapa
Related Posts:
ALICHOKIZUNGUMZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI CONGO KUHUSU MADEREVA WALIOTEKWA Jana ziliripotiwa habari za kutekwa kwa madereva wa malori kutoka Tanzania na Kenya kutekwa na kundi la waasi nchini Congo. Leo September 16 habari zilizoripotiwa na BBC Swahili zimedai kuwa watu wameokolewa na jesh… Read More
SAKATA LA REDIO KUFUNGWA MAGIC FM YATAKIWA KUOMBA RADHI SIKU TATU MFULULIZO, REDIO 5 ZAFUNGIWA MIEZI August 29 2016 Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye alitangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni Magic Fm ya Dar es salaam na Radio 5 ya Arusha kwa makosa ya kut… Read More
SERIKALI YAANZA MAZUNGUMZO YA KUWAOKOA MADEREVA 12 WALIOTEKWA CONGO Serikali imeingilia kati na kuanza mazungumzo ya kuwaokoa madereva 12 wa malori kutoka Tanzania waliotekwa nchini Kongo (DRC) na kundi la waasi wa Mai Mai.loritanzaniaWaasi hao mbali na kuwateka madereva hao wametoa saa 24… Read More
RUBBY ATANGAZA KUJISIMAMIA MWENYEWE BAADA YA KUTEMANA NA CLOUDS FM, ADAI SASA NI YEYE NA MASHABIKI WAKE Msanii wa Bongo Fleva, mwanadada Ruby ambaye amewahi kutamba na wimbo wake wa “Na Yule’ amefunguka na kusema kwa sasa amebadili uongozi wake na kujisimamia yeye kwani anataka kusimama yeye pamoja na mashabiki zake.R… Read More
ZOMBE AACHIWA HURU, MSHIRIKA WAKE AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA Mahakama ya Rufaa imemhukumu aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni kunyongwa hadi kufa katika kesi ya vifo vya wafanyabiashara wa madini iliyokuwa ikimkabili yeye pamoja na aliyekuwa Mk… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni