Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mama’ke mzazi, Sanura
Kassim ‘Sandra’ wamelazimika kukaa kikao kizito ili kupata muafaka wa
mzazi mwenzake na staa huyo, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kurejea
Bongo na kuishi katika nyumba moja na mkwewe huyo ambaye walipishana
kauli hivi karibuni.
Hivi karibuni, Zari aliyekuwa akiishi na mama Diamond nyumbani kwake,
Tegeta-Madale jijini Dar, walipishana kauli na mzazi huyo sambamba na
ndugu zake hadi kufikia hatua mrembo huyo aliyezaa mtoto mmoja na
Diamond (Tiffah) kurejea nyumbani kwake Afrika Kusini kupisha kile
alichokiita ni ‘uswahili’.
Chanzo makini kimeeleza kuwa, baada ya kuona Diamond anampenda Zari na
mapenzi yao ni motomoto, familia haikuwa na jinsi zaidi ya kukaa kikao
kulijadili kwa kirefu suala hilo na kupata muafaka ambapo habari njema
ni kwamba, mama Tiffah anatarajia kutua Bongo siku chache zijazo.
“Diamond si unajua ndiyo kichwa katika familia. Amewaita ndugu
akawaeleza dhamira na mikakati yake na Zari hivyo wamekubaliana arejee
Bongo,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo, hakutaka kufunguka kwa undani akidai ni mambo ya kifamilia.
“Kila kitu kipo sawa. Zari ataibuka na maisha yataendelea kama kawaida, haya mambo ya kifamilia bwana,” alisema Diamond.
Kabla ya kufikia muafaka huo, Zari aliripotiwa kuwa anakuja nchini
Desemba 8, mwaka huu wakati mama Diamond akionekana kupinga lakini
hatimaye muafaka umepatikana.
GPL
Jumamosi, 5 Desemba 2015
Home »
» Diamond Platnumz na Mama yake Wakaa Kikao Kizito..Kisa Zari
Diamond Platnumz na Mama yake Wakaa Kikao Kizito..Kisa Zari
Related Posts:
Harmo Rappa Azidi Kutembelea Nyota za Wasanii Wakubwa...Amchokoza AY Msanii Ay mzee wa commercial ameamua kumuachia jina lake Rapa anayekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva HamoRappa. Jina la Legend alikuwa akitumia mzee wa commercial kwenye mtandao wa Twitter lakini sasa ameliachia ra… Read More
Unatamani Kumuacha ila Unashindwa? Ngoja Nikwambie Kitu Kuna watu wana Mikwara sana, ukiachana nae anaanza Maneno ya shombo, wengine hudiriki kukwambia ''you cant live without me utarudi tu'', unajiuliza huyu mtu ana Hisa kwenye mishipa yangu ya moyo au ana mrija wa Oxygen… Read More
Mwanamke Aelezea Jinsi Askari Walivyombaka Msumbiji Wakati Serikali ikiahidi kufanya uchunguzi wa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika kutimua Watanzania nchini Msumbiji, mwanamke mmoja amesema alibakwa na askari watatu kabla ya kuwekwa mahabausu ambako ali… Read More
Hivi Ndivyo Uzuri wa House Girl Ulivyomponza Mke wa MTU Mpaka Akaambukizwa Ukimwi Inasikitisha sana. Fuatilia mkasa huu mwanzo mwisho.... Mke alimhisi mmewe kuwa anatembea na housegirl wao kutokana na ukweli kuwa, housegirl alikuwa mzuri mno kimuonekano, kiumbo na kwa sura. Alifikiri kumfukuza ila m… Read More
Ukweli Mchungu Kuhusu Anayejiita Mdogo wa Gwajima...!!!! Amejitokeza mtu mmoja na kufanya press conference kwa jina anajulikana kama Methusela Gwajima , huyu Bwana ni Mwanasheria na ameajiriwa kwenye law firm ya Francis Stolla ambaye anagombea Urais wa TLS . Huyu Mwanashe… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni