Usemi wa Waswahili kuwa, ukimwaga ugali, nami namwaga mboga umetimia kwa
klabu ya soka ya Yanga ambayo licha ya uongozi wake jana kukanusha
kuajiriwa kwa kocha Mzambia George Lwandamina na kuachana na Mdachi Hans
van der Pluijm, mzungu huyo ametangaza kujiuzulu kazi hiyo.
Mapema jana, katibu mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit alisema uongozi wao
hauna taarifa za ujio wa Lwandamina wala haujafanya mawasiliano yoyote
na mkufunzi huyo. “Kwanza, hizo taarifa nasikia kwako, hatujazungumza
naye na wala hatujui kama amekuja, anaweza kuwa amekuja kwa shughuli
zake. Kocha Yanga ni Hans Pluijm,” alisema Baraka.
Lwandamina alikanusha akisema kwamba ujio wake nchini hauna maana kwamba
amekuja kusaini mkataba Yanga, ingawa alikiri kwamba timu hiyo
inamhitaji na kama ikichangamka yuko tayari kufanya kazi nchini.
Sababu za uamuzi wa Pluijm
Akizungumza uamuzi wake wa kujiuzulu, Pluijm alisema uwapo wa kocha huyo
nchini umemchukiza na kuamua kumuandikia mwenyekiti wa klabu hiyo,
Yusuf Manji barua ya kujiuzulu nafasi yake.
Pluijm alisema hajafurahishwa na mambo yalivyokuwa yakifanyika na kwamba
licha ya uongozi wa klabu yake wakati wote kukanusha hawana mpango na
Lwandamina, lakini anao uhakika wako katika mazungumzo na kocha huyo wa
Zesco United.
Alisema kuna nafasi Yanga walitaka kumpa, lakini ameshindwa kukubaliana nayo kutokana na mambo yalivyofanyika.
Pluijm alitajwa kubadilishiwa wadhifa na kuwa mkurugenzi wa ufundi wa
klabu hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Lwandamina. “Unajua hakuna siri
katika dunia ya sasa, sijafurahi mambo yalivyokuwa yanafanyika
hawakutanguliza heshima kwangu, nimewaandikia barua ya kujiuzulu ili
waniache niondoke vyema,” alisema Pluijm na kuongeza: “Sikupanga
kuondoka Yanga kwa ubaya, lakini hili sikulifurahia, nawashukuru
wanachama na mashabiki pamoja na uongozi na wachezaji wangu kwa kunipa
nafasi ya kufanya kazi hapa na kesho (leo) nitakwenda kuwaaga wachezaji
wangu,” alisema Pluijm.
Jana asubuhi, Pluijm alisema hana nafasi ya kuzungumzia ujio wa
Lwandamina na kusisitiza kuwa kwa sasa anahitaji kutuliza akili kwani
anasubiri taarifa rasmi.
Huku akicheka Pluijm alisema: “Nimesikia mengi, yameandikwa na kusemwa
juu yangu kuondoka Yanga, lakini najiamini, mimi ni kocha mwenye
kiwango, nimefanya kazi kubwa Yanga na ninazidi kuendelea kufanya,
ingawa sishangazwi na yanayosemwa kwani vitu kama hivyo ni kawaida
kutokea duniani.
“Nimeifanyia Yanga vitu vingi tangu iliponiajiri hadi sasa, kama kuna
mabadiliko nitaambiwa na waajiri wangu, nami nitaeleza misimamo wangu.”
Wengine wanasemaje
Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja alisema kuondolewa kwa Pluijm
hashangazwi nako kwani ndivyo mpira ulivyo kokote duniani. “Hata
Mourihno (Jose) alitimuliwa Chelsea, hivyo ni kawaida ya makocha, lakini
mimi sioni udhaifu wa Pluijm naangalia mafanikio aliyowapa Yanga hadi
imecheza mashindano ya kimataifa na kufika mbali tu,” alisema Mayanja.
Mwanasoka wa zamani wa Yanga na Pan African ambaye pia ni kocha,
Mohammed Adolph ‘Rishard’ alisema timu kucheza mfululizo kwa kiwango
kile kile ni ngumu hivyo haoni sababu ya Yanga kumuondoa Pluijm.
“Sioni kama Yanga iko katika kiwango kibovu nafikiri ni uchovu kwani
hata ukiangalia Azam ndiyo tatizo linalowasumbua, timu haiwezi kucheza
misimu miwili mfululizo kwa kiwango kile kile, sasa wanapobadilisha
kocha wategemee mambo mawili, timu kuendelea kuwa kama ilivyo au kuzidi
kuporomoka zaidi,” alisema Rishard.
Jumatano, 26 Oktoba 2016
Home »
» UKOCHA: Pluijm Amwaga Mboga Yanga
UKOCHA: Pluijm Amwaga Mboga Yanga
Related Posts:
Jamani Nitoke Nnje ya Ndoa..?Nahitaji Ushauri Wenu...!!! Nimevumilia majaribu ya ndoa yamenishinda, ninaishi na mke wangu lakini hatuna furaha yaani kama tumelazimishwa! Hakuna kabisa furaha, tumejaribu kukaa chini na kujadili mara nyingi sana lakini huwa anadai haku… Read More
Exclusive..Baada ya Kutemwa Yanga,Pluijm Kutua Taifa Stars,Mpango Mzima Uko Hivi..!!! UNAAMBIWA ukiona cha nini mwenzako anasema nitakipata lini, kwani baada ya Yanga kuamua kumtema kocha wao za zamani, Hans van der Pluijm, nyota ya Mholanzi huyo imezidi kung’aa na sasa ana ofa mbalimbali kutoka ndani … Read More
Ukweli Mchungu..Uwepo wa WCB; Bongo Fleva Inachungulia Kaburi...!!! Hayo yote nayasema kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Adul Juma au maarufu zaidi kwa jina la Diamond. Siku za hivi karibuni, Diamond ameanzisha zoezi la kuwachukua wanamuziki na kuwaingiza kwenye kundi lake maarufu s… Read More
Kama Umeteseka kwa Muda Mrefu,Hizi Hapa Mbinu za Kuamsha Nguvu za Kiume Kwa Muda Mrefu..!!!! Suala la nguvu za kiume kwa sasa limeshakuwa ishu kubwa kwa vijana wengi wa sasa,kwa utafiti uliofanywa mwaka 2013 na shirika la Afya duniani unaonesha kuwa zaidi ya asilimia themanini ya wanawake hawatoshelezwi kimap… Read More
Unatamani Kumuacha ila Unashindwa? Ngoja Nikwambie Kitu Kuna watu wana Mikwara sana, ukiachana nae anaanza Maneno ya shombo, wengine hudiriki kukwambia ''you cant live without me utarudi tu'', unajiuliza huyu mtu ana Hisa kwenye mishipa yangu ya moyo au ana mrija wa Oxygen… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni