Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa amechambua
mwaka mmoja wa uongozi wa Rais John Magufuli tangu aingie madarakani
akisema kuna mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha
ya wananchi yamezidi kuwa magumu.
Lowassa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 aliungwa mkono na
vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
alisema hayo jana katika andishi lake kwa vyombo vya habari.
Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu katika Serikali ya Awamu ya
Nne kabla ya kujiuzulu mwaka 2008, amesema katika andishi hilo kwamba,
“kile ambacho tulikisema wakati ule kwa nini tunataka mabadiliko, hivi
sasa kila mtu anakiona.
“Kwamba pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini
maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri
kulipuka, elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa, utumishi wa umma
umekuwa kaa la moto.”
Jumatano, 26 Oktoba 2016
Home »
» Edward Lowassa Anena Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli
Edward Lowassa Anena Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli
Related Posts:
TETESI ZA SOKA ULAYALiverpool wapo tayari kumfuatilia tena Ryan Bertrand, 24, kutoka Chelsea, wakati Brendan Rodgers akisaka beki wa kushoto (Daily Mail) kiungo wa Borussia Dortmund Marco Reus, 25, na beki wa Southampton Dejan Lovren, 25, ni … Read More
Mwanamke wa Sudan aliehukumiwa kifo kwa kuolewa na Mkristo amewasili Italia. Huyu wa kwanza kushoto aliembeba mtoto ni Makamu wa waziri wa mambo ya nje ya Italy Lapo Pistelli Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pope Francis Alhamisi ya July 24 2014 nchini Italia amekutana na Meriam mwanamke wa S… Read More
Mnigeria aliebeba dawa za kulevya alivyokamatwa Nairobi baada ya rubani kuugua.Mwanamume mmoja Raia wa Nigeria imebidi alazwe kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta Nairobi Kenya baada ya kugundulika alikua na mzigo wa dawa za kulevya wa vidonge 57 tumboni mwake. Huyu jamaa alikua anazisafirisha hizi… Read More
NDEGE NYINGINE YAPOTEA HUKO ALGERIA Maafisa wa masuala ya anga nchini Algeria wanasema wamepoteza mawasiliano na ndege ya shirika la ndege la Air Algerie, iliyokuwa katika anga ya Sahara. Shirika la habari za Algeria limesema ndege hiyo ilikuwa ikisafiri… Read More
Ratiba ya Serengeti Fiesta 2014 imetoka mdau wangu.. Fiesta ni tamasha linalowakutanisha wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania kwenye msimu wa mafanikio pamoja na mashabiki wao kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kuna mikoa kadhaa imeongezeka. Kupitia show ya XXL, Seb… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni