Alhamisi, 24 Julai 2014

Kama ulisikia au kusoma kwamba Mama Diamond na Wema hawaelewani.

Wema na Mama Wema 2Najua kuna stori nyingine huwa zinaandikwa alafu wahusika wakuu wanakuja kuziongelea baadae kwa kushangaa kilichoandikwa ambacho mara nyingi kinakua sio cha kweli.
Stori ya Wema kutopatana na ‘mama mkwe’ yaani Mama mzazi wa Diamond ni miongoni mwa stori ambazo kuna uwezekano umeshawahi kukutana nazo kwenye Magazeti au baadhi ya mitandao, stori ambazo zilianza kuandikwa tu baada ya mastaa hawa kurudi mapenzini.
Sasa kwenye exclusive na youngluvega.blogspot.com Wema anasema ‘Watu wanasikia vitu vingi hata kwenye Magazeti watu wanaandika vitu vingi hususani Waandishi huwa wanatengeneza ili tu kupata habari lakini hatuwezi kusema kila kitu kinachotuhusu sisi kila mtu anajua….. hapana, mbona mimi na mama tunapatana tuuuu’
Wema na Diamond 1‘Mbona mami ake wangu mieeeee…. mwenyewe ananiitaga chizi langu, kwa hiyo tuko okey sana, nadhani watu wanamawazo hayo kwa sababu Mama ni mama yake Naseeb na mwisho wa siku Naseeb anakua sometimes hivi sometimes vile yeye kama mama lazima asimame nyuma ya mtoto wake ila mama yuko okey, mama ni mchizi wetu.. kamanda wetu mwenyewe.

IDADI YA JEZI ALIZOUZA JAMES RODRIGUEZ NDANI YA SAA MOJA TU.

Screen Shot 2014-07-24 at 9.33.54 AMMuda mfupi baada ya kujiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 63, mchezaji wa Colombia James Rodriguez ameweka rekodi katika mauzo ya jezi yake ya Real Madrid.
Ripoti za Hispania zinasema Jezi zipatazo 900 za James Rodriguez ziliuzwa ndani ya ndani ya saa moja tangu zilipoingia rasmi sokoni ambapo zimeuzwa kwenye duka la Real Madrid na imeonyesha kiasi gani raia huyu wa Colombia anavyokubalika. Rodriguez ametua Madrid akitokea AS Monaco huku akiwa ndiye mfungaji bora wa Kombe la Dunia nchini Brazil 2014 baada ya kutokana na magoli 6 aliyofunga.

Jumatano, 23 Julai 2014

Hospitali ya Muhimbili imesemaje kuhusu mabaki ya binaadamu Tegeta?

Jeshi la Polisi linawahoji watu nane wakiwemo Madaktari wa chuo cha kitabibu cha IMTU kwa madai ya kutupa mabaki ya masalia ya binadamu katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji kata ya Mbweni wilayani Kinondoni Dar es salaam.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema kulipatikana mifuko 85 iliyobeba mabaki ya masalia hayo ya binadamu.
‘Imeonekana mara ya mwisho viungo hivyo vilikua katika chuo cha Udaktari cha IMTU kinachofundisha kwa vitendo pia, sasa tunachunguza na wamekubali kuhojiwa, maswali yanayofata ni kwanini viungo hivyo vilikua pale kwa wingi kiasi hicho? kwa nini vilikwenda kutupwa? ‘ – Kova
Screen Shot 2014-07-24 at 3.44.25 AMKwenye hii ishu pia hospitali ya taifa Muhimbili inachunguzwa ambapo mkuu wa kitengo cha uhusiano kwenye hospitali hii ya taifa Aminiel Aligaesha amesema >> ‘Sisi ni miongoni mwa wanaochunguzwa kwa sababu ni hospitali mojawapo katika jiji la Dar, mabaki yale hayakutoka hospitali ya taifa Muhimbili’
‘Kuharibika kwa tanuru letu la kuchoma taka za kitabibu kama hizo hakuna uhusiano na mabaki ya binadamu yaliyookotwa Tegeta, ni kweli tanuru liliharibika February 2014 na mwezi April tukapata spea lakini tatizo jingine likatokea na kipuri kingine kikaagizwa na mpaka sasa mafundi wanaendelea kuitengeneza’ –Na mimi Nickson Luvega.

Kilichoendelea kesi ya Mbasha Mahakamani July 23 2014, kakubali sentensi mbili tu.

KESI ya ubakaji inayomkabili mume wa Flora Mbasha ambae ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Tanzania Emmanuel Mbasha (32), ilitajwa tena July 23 2014 katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo Mbasha amesomewa tena mashataka yake huku akikubali sentensi mbili tu kati ya nne zilizosomwa.
Akisoma hoja hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago, mwendesha mashtaka wa serikali Nasoro Katunga alisema May 23 2014 mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye  Yerusalemu Boazi (17) ambae ni mdogo wa Flora na kumlazimisha asimwambie mtu yoyote ambapo wakati akitenda kosa hilo mkewe Flora hakuwepo nyumbani.
Katunga aliendelea kufafanua kuwa May 25 2014 Mbasha alirudia tena kitendo cha ubakaji baada ya kumuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambae hakuwepo nyumbani ambapo walipofika Tabata peke yao, Mbasha alimbaka tena binti.
Hizo sentensi zote mbili za juu Mbasha amezikana Mahakamani kwa kusema sio kweli.
Hata hivyo iliendelea kuelezwa kwamba tukio hilo la ubakaji liliripotiwa katika kituo cha polisi Tabata ambako Boazi alipewa PF3 kwa ajili ya kupata matibabu ambapo uchunguzi uliofanywa ulionyesha ni kweli binti huyo aliingiliwa kimwili.
Mbasha 25
Mbasha akiwa na baba yake mzazi Mahakamani.
Katika kesi hiyo ambayo Mbasha anatetewa na wakili Mathew Kakamba, Mbasha alikubali sentensi mbili na kuzikataa mbili zilizobaki kwamba alimbaka binti huyo.
Alichokubali ni kusema ni kweli alimuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambaye hakuwepo nyumbani na pia alikubali ni kweli Mei 23 2014 mke wake Flora Mbasha hakuwepo nyumbani.
Baada ya kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashataka wa serikali, Jaji Luago aliahirisha kesi hiyo hadi August 22 2014 baada ya wakili anayemtetea Mbasha kudai atakuwa na safari kwa siku za karibuni nje ya Mkoa.

Real Madrid yamsajili mkali wa mabao James Rodriguez

rodr
Real Madrid wamekamilisha usajili wa mshindi wa kiatu cha dhahabu katika michuano ya World cup ndani ya Brazil 2014. James Rodriguez
mshambuliaji  kutoka Colombia ana umri wa miaka 23 na amesaini mkataba wa miaka sita na Real Madrid akitokea club ya  Monaco.


Ripoti zinasema gharama ya uamisho ni pauni milioni 63 na kumfanya mchezaji wa nne wa uhamisho wa gharama akiwa nyuma ya Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.


Kama umesahau ni kwamba Rodriguez alifunga magoli sita katika mechi tano za world cup hadi kuifikisha timu yake ilipofika katika robo fainali. Picha hapo chini ni  James Rodriguez akiwa katika vipimo vya afya Real Madrid.

kk

Baada ya Davido kuambiwa anajionyesha na mali zake kwenye instagram..amejibu kama ifuatavyo..

dadivoMsanii staa wa Nigeria Davido ni mtu ambae huwa anaonyesha kwenye mitandao vitu vingi anavyonunua mfano saa za Rolex za dhahabu, magari ya kifahari, nyumba na vitu vingine ambapo baada ya kuulizwa kuhusu ishu hii ya kupenda kuonyesha mali zake amejibu “sitoweza kusema kama ni kujionyesha kwa mali zangu, yale ni magari yangu, zile pesa zangu na pia ile ni page yangu’
Sio lazima unifollow kwenye instagram wala kunifata kwenye mtandao wowote wa kijamii, ingekuwa tofauti sana kama nataka kujitangazia mali zangu basi ningetumia mabango ya barabarani lakini sifanyi hivyo.
wwwwwwwwwwwwwwwUnadhani ni sahihi kwa mastaa kuonyesha mali zao na pesa kama hivi kwenye mitandao ya kijamii? niachie comment na like yako hapa chini mtu wangu ili twende pamoja.

Picha za actors 10 waliotajwa na Forbes kwa kulipwa pesa nyingi 2014

dola
Forbes.com kwa wakati huu wametoa list ya mastaa 10 wa kiume ambao wamelipwa pesa nyingi zaidi kwenye kazi zao za filamu. Muigizaji mweusi ni Will Smith peke yake kwenye top 10 wengine wote ni wazungu.
1 Robert Downey Jr – $75 million
2
2 Dwayne Johnson – $52 million
1
3 Bradley Cooper  – $46 million
3
4 Leonardo DiCaprio – $39 million
4
5 Chris Hemsworth – $37 million
6
6 Liam Neeson – $36 million
l
7 Ben Affleck – $35 million
5
8 Christian Bale – $35 million
chris
9 Will Smith – $32 million
dd
10 Mark Wahlberg – $32 million
dfff