Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema kulipatikana mifuko 85 iliyobeba mabaki ya masalia hayo ya binadamu.
‘Imeonekana mara ya mwisho viungo hivyo vilikua katika chuo cha Udaktari cha IMTU kinachofundisha kwa vitendo pia, sasa tunachunguza na wamekubali kuhojiwa, maswali yanayofata ni kwanini viungo hivyo vilikua pale kwa wingi kiasi hicho? kwa nini vilikwenda kutupwa? ‘ – Kova
‘Kuharibika kwa tanuru letu la kuchoma taka za kitabibu kama hizo hakuna uhusiano na mabaki ya binadamu yaliyookotwa Tegeta, ni kweli tanuru liliharibika February 2014 na mwezi April tukapata spea lakini tatizo jingine likatokea na kipuri kingine kikaagizwa na mpaka sasa mafundi wanaendelea kuitengeneza’ –Na mimi Nickson Luvega.
0 comments:
Chapisha Maoni