Jumanne, 5 Agosti 2014

Umeipata hii ya Weusi kusemekana wamecopy wimbo?

we
Kupitia You heard ya August 04,Weusi wamesemekana kucopy wimbo na kuurudia kuanzia namna wanavyorap mpaka beat iliyotumika kwenye wimbo huo,Joh Makini kaongea na kapatikana pia producer wa wimbo huo NahReel nae kazungumza.
88.0 Clouds Fm inasikika ukiwa Tabora.
Bonyeza play kusikiliza.

Sina muda kujadili upuuzi huu kuhusu Ridhiwani – Rais Jakaya Kikwete

kikwere
Taarifa kutoka ofisi ya Rais kuhusu maneno yanayosemekana kwamba Rais Jakaya Kikwete kushiriki kusaidia kumwokoa mwanae ambaye ni mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete baada ya kukwamatwa na dawa za kulevya nchini China.
Hii ni taarifa kutoka ofisi ya Rais yenye maneno ya Rais Jakaya Kikwete.
k1
k2

Magazine yamuomba msamaha 2 Face Idibia baada ya kesi ya Naila milioni 100.

idibiaIcon Weekly magazine walitoa habari kwamba 2 Face Idibia ametoka nje ya ndoa yake na kuanzisha uhusiano na mfanyakazi wa benki. Magazine hiyo haikuishia hapo iliendelea kusema kwamba 2 face amempa ujauzito mwanamke huyo.
Habari hiyo ilimchafua 2 face kwasababu yupo ndani ya ndoa na ndio ilikuwa habari kubwa ya magazine kwa kuwekwa mbele ya cover. Baada ya magazine kutoka 2 face alifungua mashtaka dhidi ya magazine hiyo kwa kudai fidia ya Naila millioni 100.
Baada ya magazine kushindwa kuthibitisha habari hiyo wametumia page moja nzima ya tolea jipya kumuomba msamaha 2 face. Japokuwa Idibia hajajibu hadharani kuhusu msamaha huo, taarifa zinasema kwamba amekubali maombi yao.
e

Yaliyoikuta Yanga Kagame Cup baada ya kupeleka kikosi cha Pili

DSC_0082-1Baada ya jana usiku katibu mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Nicholas Musonye kutoa onyo kwa Yanga kuwasilisha majina mapya ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya Kagame Cup, leo hii CECAFA wametoa uamuzi mpya dhidi ya Yanga.
Yanga SC sasa rasmi imeondolewa kwenye michuano ya Kagame kutokana na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati kupinga kupeleka timu ya vijana.
Yanga ilitaka kupeleka timu yenye vijana wengi iliyochanganyika na wakongwe wachache.
Lakini Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye akasema hizo ni dharau. Wanasema ni timu ina wachezaji wa timu ya kwanza, vipi Maximo abaki Dar es Salaam.
“Halafu timu isafiri kwenda kwenye mashindano makubwa kama ya Kagame. Huu ni utani, ndiyo maana sasa tumeipa nafasi Azam,”alisema jana.
Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC, watapambana Kundi A lenye timu za Rayon Sport ya Rwanda, Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya Sudan Kusini na KMKM ya Zanzibar.
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, KCC ya Uganda, Flambeau de L’Est ya Burundi, Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti wakati Kundi C linaongozwa na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi, El Merreikh ya Sudan, Polisi ya Rwanda na Benadir ya Somalia.
Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye mlezi wa mashindano haya ambaye hutoa dola za Kimarekani 60,000 kila mwaka kwa ajili ya zawadi.
Kwa kuwa Azam imechukua nafasi ya Yanga, sasa itacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya wenyeji Rayon Sport Uwanja wa Amahoro Agosti 8, mwaka huu.
Mechi ya saa 8 mchana itakuwa ni kati ya KMKM ya Zanzibar  dhidi ya  Atlabara ya Sudan Kusini. 
Mechi ya pili ya Azam FC itakuwa  Agosti 10 dhidi ya KMKM, kabla ya kuivaa Atlabara Agosti 12, halafu itamaliza makundi dhidi ya Coffee ya Ethiopia Agosti 16.

Jumapili, 27 Julai 2014

Taarifa rasmi kutoka club ya Chelsea kuhusu Didier Drogba.

Screen Shot 2014-07-25 at 9.05.55 PM 
Utakua uliziona tu zile headlines za mitandao na magazeti mbalimbali duniani kuhusu uwezekano wa staa huyu wa soka Didier Drogba kurejea kuichezea Chelsea baada ya Jose Mourinho kuonyesha nia ya kumrudisha.
Sasa taarifa rasmi iliyothibitishwa na Chelsea, mzaliwa huyu wa Ivory Coast amerejea rasmi kwenye club hii kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo wakati akitia saini, Drogba amesema ‘ulikua ni uamuzi rahisi kabisa wa kuamua kufanya tena kazi na Jose Mourinho, kila mmoja anajua uhusiano wangu na hii club… imekua ni kama nyumbani’
Jose Mourinho mwenyewe amesema ‘amerudi kwa sababu ni mmoja wa wachezaji bora Ulaya, namjua vizuri… na amekuja kuiweka historia nyingine’
Drogba ameifungia Chelsea magoli 157 kwenye mechi 342 alizotokezea.
Screen Shot 2014-07-25 at 9.13.00 PM

Video mpya ya Barnaba aliyoonekana na mke wake ndio hii.

Screen Shot 2014-07-26 at 2.30.12 AM
Hii single inaitwa ‘Wahaladee’ ambayo ni miezi kadhaa imepita tangu utoke rasmi kwenye Radio lakini July 25 2014 Watanzania wameletewa video yake ambayo imeongozwa na Nick Dizzle ambapo kingine kikubwa kwenye hii video ni mrembo alieigiza ndani yake, ni mke wa ndoa wa Barnaba (Mama Steven)
Naambiwa video imefanywa Kenya na Tanzania.

Matokeo ya tuzo za AFRIMMA 2014 alizokua anawania Diamond Marekani.

Screen Shot 2014-07-27 at 9.43.50 AM 
Zinaitwa African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo.
Good news za ushindi wote huu ni kwa mujibu wa meneja Babu Tale ambae nae kahudhuria tuzo hizi Marekani alienitumia msg kwa kusema Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa Nigeria.

Kolabo bora ni tuzo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru na Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow down’
Tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na Jackie Gosee wa Ethiopia.
Screen Shot 2014-07-27 at 8.17.01 AM 
Lady Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki aliyokua anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya, Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.
Producer bora wa mwaka tuzo yake imechukuliwa na Mtanzania Sheddy Clever aliekua anashindana na Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash Wonder wa Uganda na Ogopa wa Kenya.
Tuzo ya Mtayarishaji bora wa video imekwenda kwa Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya ‘My number 1′ ya Diamond Platnumz.
Screen Shot 2014-07-27 at 8.17.33 AM
Tuzo zenyewe zimetolewa kwenye hili jengo
Stori zaidi na pichaz vitafata baadae hivyo endelea kukaa karibu na millardayo.com mtu wangu ili ujue kilichotokea kwenye tukio hili ambalo limewahusisha wakali wengine kama Davido, 2Face, Fally Ipupa, Iyanya, Flavour, Wyre, Miriam Chemmoss na wengine ambao ni sehemu ya watu kutoka nchi 17 za Afrika.