Serikali ya Ujerumani imeeleza kufurahishwa na kasi ya kupambana na
rushwa na ufisadi ya Rais John Magufuli na kuahidi kumpa ushirikiano
katika masuala ya maendeleo.
Ujerumani inakuwa nchi ya kwanza ya kigeni kuvutiwa na kasi ya Rais
Magufuli ambaye ameonekana kuelekeza nguvu katika si tu kupambana na
maovu hayo tangu aapishwe Novemba 5, bali pia kuchochea maendeleo ya
watu wenye kipato cha chini.
Aidha, Ujerumani imesema inasubiri kuona vipaumbele vya maendeleo
vitakavyoainishwa na serikali ya Rais Magufuli ili iweze kuisaidia
utekelezaji.
Pongezi hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani, Georg Schmidt.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yake ya siku tano hapa
nchini, Schmidt alisema katika kipindi cha mwezi mmoja tu, Dk. Magufuli
ameweza kushughulikia masuala muhimu ya kijamii ikiwamo kuboresha huduma
za afya na kuwashughulikia wakwepa kodi.
Kasi ya Rais Magufuli, alisema, itasaidia kuokoa fedha nyingi ambazo
zitakapokusanywa zitachangia miradi mbalimbali ya maendeleo kama
alivyofanya tayari kwenye afya na elimu.
Mkurugenzi huyo alisema ziara yake nchini ilikuwa na lengo la kuangalia
hali ya maendeleo nchini baada ya uchaguzi, miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na serikali yake pamoja na kukuza ushirikiano baina ya
nchi mbili hizo.
Alisema ameshakutana na baadhi ya watendaji wa serikali, wabunge,
wanaharakati, watendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na
kuitembelea Mahakama ya Haki za Binadamu iliyopo mjini Arusha.
Alisema pia amekuja kuangalia fursa za kibiashara nchini kwa sababu
wawekezaji wengi duniani huvutiwa kwenda kuwekeza kwenye mataifa
mbalimbali iwapo nchi hiyo ina usalama wa kutosha.
Akizungumzia suala la Zanzibar, Schmidt aliwataka wananchi kuwa na
subira wakati mazungumzo yakiendelea katika jitihada za kutatua mgogoro
huo.
“Mazungumzo yanaendelea ya usuluhishi tunasisitiza utulivu, amani na tuna imani mwafaka mzuri utafikiwa,” alisema.
Alisema kwa sasa serikali ya Ujerumani itazielekeza fedha nyingi kwa
serikali ya Tanzania ili kushughulikia wakimbizi kutoka Burundi
wanaokimbia machafuko.
“Tuna jukumu na wajibu wa kushughulikia mgogoro wa Burundi na fedha
zilizokuwa zinakwenda Burundi sasa zitaelekezwa Tanzania kwa kuwa
wanapokea wakimbizi wengi zaidi,” alisema Schmidt.
Jumapili, 6 Desemba 2015
Home »
» Ujerumani Yamsifu Rais Magufuli Kwa Kupambana na Ufisadi Kwa Vitendo.....Yaahidi Kumpa Ushirikiano
Ujerumani Yamsifu Rais Magufuli Kwa Kupambana na Ufisadi Kwa Vitendo.....Yaahidi Kumpa Ushirikiano
Related Posts:
Mdahalo Wa Tahliso Kujadili Hotuba ya Magufuli Waingia Dosari Baada Ya Wanafunzi wa UDSM Kuupinga WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye jana alinusuru kuvunjika kwa mdahalo ulioandaliwa na Jumuiya ya Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO), baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Sa… Read More
Waziri Atoa Mkwara Jeshi la Polisi Atoa Siku Mbili Aletewe Taarifa Kuhusu Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Watu Kubambikiwa Kesi Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga amefanya ziara ya ghafla leo Dec 16 2015 katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Polisi Dar es salaam na kutoa amri kwa viongozi wa jeshi hilo siku mbili za kuhakikisha amepata ta… Read More
Chadema Bado Hawajakubali Yaishe...Waapa Kumshughulikia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Bungeni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia Bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai kuwa bado hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya Escrow. Ahadi hiyo il… Read More
Nape: Nitaanza Kushughulikia Sheria na Nidhamu Michezoni Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameahidi kushughulikia sheria mbalimbali zinazosimamia sekta hiyo ili kuongeza nidhamu michezoni. Nape aliyeapishwa juzi kuanza kibarua hicho, ataiongoza wi… Read More
Asipofunga Zipu…Nay wa Mitego Atakufa Kwa Ngoma Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’ akijiachia na mrembo mpya mwenye umbo dogo kwenye bwawa la kuogelea katika Hoteli ya White Sands iliyopo Mbezi Beach jijini Dar. KIWEMBE! Ndivyo… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni