Chipukizi
 wa Bongo flava anayeunguruma poa na hit yake ‘Aiyola’, Harmonize 
amesema waongozaji wa video za muziki kutoka Afrika kusini huwa 
wanaonesha heshima ya hali ya juu wanapokutana na wasanii kutoka 
Tanzania.
Akifunguka
 mbele ya kipaza sauti cha Timesfm.co.tz, Mkali huyo ambaye jina lake 
halisi ni Rajab amedai sababu kubwa ya kupewa heshima ni kwa kuwa mziki 
wetu ni wa pili kwa ukubwa Barani Afrika ukiwatoa Nigeria.
“Labda
 mi niseme kitu kimoja” alisema “Directors wa kule(Afrika kusini) 
wanajua kabisa ili uweze kuhit Afrika mashariki ni lazima utusue 
Tanzania, na hilo liko wazi sisi ni wa pili kimuziki Afrika na 
tunaushindani mkubwa na Nigeria tu.







 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni