Rais Magufuli amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato 
Tanzania Dkt. Philip Mpango kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato 
inayofanywa na mamlaka hiyo ambayo imeongeza ukusanyaji wa Mapato na kwa
 mara ya kwanza mwezi huu ukusanyaji wa mapato hayo unatarajiwa kuwa 
zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 300
Kutokana na mafanikio hayo amewahakikishia watanzania kuwa fedha kwa 
ajili ya kutimiza ahadi ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi na 
sekondari ambazo ni kiasi cha shilingi Bilioni 131 zitatengwa mwezi huu 
na kupelekwa moja kwa moja katika shule husika.
Amesema wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa 
watapatiwa nakala za taarifa za ugawaji wa fedha hizo na kuonya kuwa 
hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kuzitumia vibaya.
Dkt. Magufuli ameongeza kuwa fedha hizo ambazo ni pamoja na fedha za 
maendeleo, fedha za mitihani na fedha vifaa vya kufundishia zitaanza 
kutumwa kila mwezi kuanzia mwezi huu wa kumi na mbili.







 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni