Ijumaa, 18 Novemba 2016

Je, Paul Makonda Anajua Mantiki ya Alichosema Kuhusu Waliotaka Kumuhonga Mil 50 Kisheria?

Kwanza nianze kwa kusema kuna mambo mengi ninakubaliana na utendaji wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lakini kuna mambo machache ambayo yananipa ukakasi unaonifanya nitimize wajibu wangu kama raia katika kumkosoa, kumuelimisha na kumjenga zaidi katika utendaji wake kama Mkuu wa Mkoa.

Jambo moja ambalo linapelekea msingi wa mada yangu ni kuhusu hii kauli yake aliyonukuliwa akisema,
"Kuna kikundi cha watu kumi ambao hao walikuja kwangu na mimi niliamua kuwatambua kama maajenti wa shetani, walikuja kwangu wanapata faida kati ya milioni 35 mpaka 45 kwa mwezi, wao walio kumi wakakubali kupanga mkakati eti wa kunishawishi nikubali niwe napokea milioni tano tano kwa mwezi kwa watu kumi maana yake milioni 50. Nikae kimya nisipige kelele juu ya shisha ili wao waendelee kupata faida".

Hii kauli ukiichambua katika msingi wa lateral thinking huwezi kugundua impact iliyobeba hasa ikichukuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Mkuu wa Mkoa kama mwakilishi wa Rais wa Tanzania ambaye pia Rais ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama lazima aelewe kuwa sheria ya kupambana na rushwa katika kifungu cha 39(1-2) inamtaka aijulishe TAKUKURU kama anadhani kuna matendo ya rushwa.

Kifungu cha 39(1) kinasema;
39.-(1) Every person who is or becomes aware of the commission of or the intention by another person to commit an offence under this Act shall be required to give information to the Bureau.

Kama hiyo haitoshi, Makonda lazima aelewe kuwa soliciting bribes ni kosa la jinai ambalo limefafanuliwa katika kifungu cha 15(1a-b) ya sheria ya The Prevention and Combating of Corruption Act 2007.

Moja ya vifungu vya Sheria inasema;
15.-(1) Any person who corruptly by himself or in conjunction with any other person-
(a) solicits, accepts or obtains, or attempts to obtain, from any person for himself or any other person, any advantage as an inducement to, or reward for, or otherwise on account of, any agent, whether or not such agent is the same person as such first mentioned person and whether the agent has or has no authority to do, or forbearing to do, or having done or forborne to do, anything in relation to his principal’s affairs or business; or

(b) gives, promises or offers any advantage to any person, whether for the benefit of that person or of another person, as an inducement to, or reward for, or otherwise on account of, any agent whether or not such agent is the person to whom such advantage is given, promised or offered and whether the agent has or has no authority to do, doing, or forbearing to do, or having done or forborne to do, anything in relation to his principal’s affairs or business, commits an offence of corruption.

(2) A person who is convicted of an offence under this section, shall be liable to a fine of not less than five hundred thousand shillings but not more than one million shillings or to imprisonment for a term of not less than three years but not more than five years or to both.

Hoja ya msingi hapa ni kutaka kufahamu kama Mkuu wa Mkoa, Makonda ametoa taarifa hii TAKUKURU? Kama alitoa taarifa, kwa nini hakuweka mtego wa kuwakamatisha kwa TAKUKURU.

Kama hajatoa taarifa rasmi, kwa nini hajatoa wakati sheria inamtaka afanye hivyo achilia mbali yuko ndani ya serikali ambayo imelifanya tatizo la rushwa kama ni kipaumbele cha kwanza katika kuwatumikia Watanzania?

Makonda hafahamu kuwa kukaa kimya bila kutoa taarifa kwenye vyombo husika kunamfanya avunje sheria kama ilivyoainishwa kwenye Penal Code CAP 16 Chapter V na pia sheria ya kupambana na rushwa ambayo imeaninishwa katika kifungu cha 30 kinachosema;
30. Any person who aids or abets another person in commission of an offence under this Act commits an offence and shall be liable on conviction to a fine not exceeding two million shillings or to imprisonment for a term not exceeding two years or to both.

Makonda hafamu kuwa sheria hazina siasa pamoja na kwamba siasa wakati mwingine hazina sheria?

Makonda kama Mkuu wa Mkoa anatakiwa awe mfano kwa wananchi wake katika kuwafichua wavunja sheria lakini anachokifanya kwa sasa ni kuwaficha wavunja sheria huku akicheza mchezo wa kisiasa.

Makonda timiza wajibu wako wa kuwafichua wahalifu kama Raia na Mkuu wa Mkoa lakini pia unatakiwa ufahamu ukubwa na umuhimu wa madaraka uliyopewa katika kuwatumikia wananchi.

Makonda naomba uwataje waliotaka kukupa rushwa ya milioni 50 ili watanzania wawafahamu kwa sababu wana haki kikatiba kuwafahamu.

0 comments:

Chapisha Maoni