Upelelezi wa kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion
anayetuhumiwa kumsababishia upofu wa kudumu Saidi Mrisho umekamilika na
hatimaye shauri hilo litasomwa Novemba 30 mwaka huu katika mahakama ya
manispaa ya Ilala.
Njwete anatarajiwa kusomewa mashtaka yake baada ya yale ya kwanza
kufutwa ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kusikilizwa baada ya
kufunguliwa mashtaka mapya.
Huyu ndiye Scropion, kijana aliyejizolea umaarufu ambapo watu wengi
hupenda kumshuhudia kila aingiapo na kutoka mahakamani huku kila mmoja
akizungumza lake kwa kesi inayomkabili.
Alipoingia mahakamani leo, aliomba ufafanuzi wa wazi juu ya mashtaka
yanayomkabili ambapo upande wa jamhuri kupitia kwa wakili wake Chesensi
Gavyole walisema ushahidi umekamilika.
Kutokana na kuombwa ufafanuzi, Hakimu anayesimamia kesi hiyo Flora Haule
amesema baada ya upelelezi huo kukamilika kesi hiyo itasomwa Novemba 30
mwaka huu, hivyo mshtakiwa atapata ufafanuzi wa mashtaka yake .
Ikumbukwe kwamba Oktoba 19 mwaka huu, Salum Njwete maarufu kama Scropion
alifutiwa kesi na kisha kusomewa upya mashtaka yake kutokana na uamuzi
wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliyeomba kufanya hivyo baada ya hati ya
awali kuwa na mapungufu ya kisheria
Ijumaa, 18 Novemba 2016
Home »
» Taarifa Kuhusu Kinachoendelea Kwenye Kesi ya Scorpion Mtoa Macho Mahakamani
Taarifa Kuhusu Kinachoendelea Kwenye Kesi ya Scorpion Mtoa Macho Mahakamani
Related Posts:
Kajala: Sijawahi Kuwa na Mahusiano ya Kimapenzi na Paul Makonda Msanii wa filamu za kibongo, Kajala Masanja amevunja ukimya na kufunguka kuhusu maneno yaliyokuwa yanazunguka mwa muda mrefu mitaani yakimtaja kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa nyakati tofauti na Mkuu wa Mkoa wa… Read More
Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya Kafeina ni nini?:1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’.Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni… Read More
BAADA ya WCB Kutoa Wimbo , Ommy Dimpoz Atao Mapovu, Diamond Amjibu na Kuvujisha Siri ya Ugomvi Wao Hii baada ya domo na mavoko kuachia ngoma povu likamtoka ommy akimshushia domo kuwa aache mziki wa ujanja ujanja akimanisha kuwa domo aache tabia zake za kununua view, tunzo kuwa awekeze kwenye mziki mzuri usio… Read More
Nimekuta Mafuta ya KY na Babcare Kwenye Mkoba wa Mchumba Wangu Ni jambo limenishangaza kifupi sina tabia ya kumfuatilia mpenzi wangu iwe kwenye simu au kwenye mambo mengi but hii ilinibidi tuu. Wakati mchumba wangu alipokuja kwangu weekend hii na kushinda siku tatu nikajit… Read More
VIDEO Mpya: Mabibi na Mabwana.. Tumealikwa Kuitazama Mpya ya Rich Mavoko ft. Diamond WCB wanayofuraha kutualika kuitazama video mpya ya kijana wao Rich Mavoko ambayo kamshirikisha Boss wake Diamond Platnumz, ukishamaliza kuitazama video hii ni ruhusa kuacha na comment yako umeionaje na wimbo we… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni