Jumatano, 2 Julai 2014

Malalamiko ya Shilole kuhusu Dj wa Club anayetaka kumdhulumu Laptop yake.

Kutoka kwa Soudy Brown kupitia You heard ya leo Shilole amelalamika juu ya mtu anayedai kumuazima laptop yake lakini anaonekana ana dalili za kumdhulumu baada ya simu zake kuwa hapokei, amemtaja kwa jina la Dj Ommy Crazy ambae ni Dj wa Club.

Bonyeza play kusikiliza.

Jinsi Beyonce alivyobadilisha mistari ya wimbo wake jukwaani kufuatia matatizo ya ndoa yake.

Wanandoa Beyonce na Jay Z wamekuwa wakipambana na uvumi kuwa sasa ndoa yao iko juu ya mawe kutokana na matatizo makubwa yanayoendelea tangu kusambaa kwa video ikimuonyesha dada wa Beyonce Solange akimshambulia Jay Z.
Na sasa Beyonce amezidi kupalilia moto zaidi kuhusiana na uvumi huo baada ya kubadilisha mistari kwenye wimbo wake kuhusu usaliti wakati akiwa jukwaani aki “perfom” kwenye ziara ya muziki na mume wake ya On The Run mjini Ohio.

Nyota huyo wa muziki wa R&B amesema kuwa Jay Z anaweza kuwa sio mwaminifu wakati akiimba wimbo wake uliotoka mwaka 2008, Resentment, ili kuendana na matukio yanayoendelea katika mahusiano yake na mumewe

Imekuwa ikivumishwa kuwa Jay Z yupo katika mahusiano ya nje ya ndoa na mwanamuziki Mya wakati wote si Jay wala Mya aliyejibu tuhuma hizo ambapo mashabiki wameendelea kuwafutilia kwa karibu hasa muziki wa Beyonce.

Angalia magoli 10 bora ya kombe la dunia – Messi vs Van Persie nani katisha?

Michuano ya kombe la dunia ipo kwenye hatua ya robo fainali ambayo itaanza rasmi Ijumaa hii. Michuano hii ya mwaka huu imekuwa na magoli mengi na bora katika historia ya michuano hii mikubwa kabisa katika soka.
youngluvega.com inakuletea video ya magoli 10 bora ya kombe la dunia kwenye hatua ya makundi.


Dar es salaam Julai 02, 2014, Gari hili la Magereza lapigwa risasi likiwa na wafungwa ndani.

Taarifa za awali zinadai kuwa Basi lililokuwa limebeba wafungwa limeshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana eneo la Mayfair Mikocheni jijini Dar es salaam.

Basi hili lilikuwa likitokea mahakama ya Mwanzo Kawe ambapo kwasasa Basi hilo liko polisi Osterbay na wafungwa hao ndani yake.
Picha zote ni kutoka Ukurasa wa Twitter wa @Switi soleji

Taarifa ya Kaimu Balozi wa Libya, Tanzania aliyejiua kwa kujipiga risasi.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania leo imepokea taarifa kutoka ubalozi wa Libya nchini ikieleza kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya Bw. Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.

Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Libya ambapo imeelezwa kuwa marehemu alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.

Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlio wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini na kuamua kumkimkimbiza hospitali ya AMI iliyopo Oysterbay ambako alitangazwa kuwa amekwishafariki dunia, kifo ambacho kimethbitishwa pia na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu Nwairat umehamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili na kwa sasa ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wake kwenda nchini Libya kwa mazishi.

Mwanaume aliyebakwa baada ya kupanda lifti ya mtu asiyemjua.

Mwanaume mmoja amebakwa katika barabara ya daraja lenye shughuli nyingi mjini Newcastle baada ya kukubali kupanda lifti ya mtu asiyemjua.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 24 aliingia kwenye gari hilo dogo mapema alfajiri ambapo alifanyiwa kitendo hicho cha ubakaji katika eneo lenye nyasi nyingi karibu na daraja la Redheugh, Newcastle.

Timu ya uchunguzi wa makosa ya ubakaji hivi sasa inaendesha msako wa mtu aliyetekeleza kitendo hicho na kuwataka mashuhuda kujitokeza hadharani.

Afisa upelelezi kutoka mji wa Newcastle, Caroline Ord, amesema hili ni tukio baya zaidi kutendewa kwa kijana huyo ambapo sasa polisi wanafanya kazi bega kwa bega na mtu huyo kuhakikisha wanampata aliyetenda kosa hilo.

Mwanamke aliyelazimika kunyoa kipara baada ya nywele zake bandia kunasa kwenye Super glue.

Mwanamke mmoja Alexis Stanton amelazimika kunyoa nywele zote kichwani baada ya nywele zake bandia kunasa kwenye gundi aina ya super glue.

Mwanamke huyo alilazimika kubaki na kipara na majeraha kidogo ambapo amesema alifanya hivyo baada ya kujikuta nywele zake alizokuwa amebandika kichwani kunasa kwenye gundi ambayo ilishindikana kutoka.

Mwanamke huyo kutoka Newcastle anasema kuwa bado anahisi maumivu kwenye kichwa chake na kwamba amelia sana tangu tukio hilo lilipotokea na bado yupo kwenye majonzi makubwa

Amesema polisi wanamsaka mtaalamu wa saluni aliyemtengeneza nywele zake mara ya mwisho ambaye aliamini anajua kazi yake lakini badala yake alimwekea super glue badala ya gundi inayotakiwa kugandishia nywele zake.