Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania leo imepokea taarifa kutoka ubalozi wa Libya nchini ikieleza kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya Bw. Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.
Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Libya ambapo imeelezwa kuwa marehemu alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.
Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlio wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini na kuamua kumkimkimbiza hospitali ya AMI iliyopo Oysterbay ambako alitangazwa kuwa amekwishafariki dunia, kifo ambacho kimethbitishwa pia na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu Nwairat umehamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili na kwa sasa ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wake kwenda nchini Libya kwa mazishi.
Jumatano, 2 Julai 2014
Home »
» Taarifa ya Kaimu Balozi wa Libya, Tanzania aliyejiua kwa kujipiga risasi.
Taarifa ya Kaimu Balozi wa Libya, Tanzania aliyejiua kwa kujipiga risasi.
Related Posts:
Angalia Thamani yako, Yanini Kumng’ang’ania Asiyekupenda? Ili mapenzi yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika mahusiano, huwa ni vyema kila mmoja kuiona thamani ya mwenzake. Ukipenda kujiangalia mwenyewe si ajabu mwenzako kupata hisia za kuwa humthamini wala humj… Read More
Jaji Chande Apewa Kazi Umoja wa Mataifa..!! Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande ameteuliwa kuongoza jopo la wataalamu watakaochunguza mazingira yaliyosababisha ajali ya ndege iliyomuua aliyekuwa katibu mkuu wa umoja huo, Dag Hammarskjold. Uteuzi huo wa jaji mkuu … Read More
Vita Dhidi ya Madawa ya Kulevya..Wanawake Wawili Wadakwa na Kilo 114 za Bangi..!! Wanawake wawili ni miongoni mwa watu zaidi ya 15 waliokamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya mkoani Mwanza Watu hao wamekamatwa wakijihusisha nadawa hizo ndani ya wiki moja kuanzia Febuari 6. Habar… Read More
RAIS DKT MAGUFULI ATEUA MABALOZI SITA KUWAKILISHA TANZANIA NCHI MBALIMBALI … Read More
Gambia bado kwa moto, Adama Barrow kaapishiwa Urais akiwa nje ya nchiAdama Barrow ambaye ni mwanasiasa wa upinzani ambaye inaaminika ndie mshindi wa uchaguzi wa Urais Gambia ameapishwa kuwa Rais wa Gambia japokua uapisho wake umefanyika nje ya taifa hilo. Uapisho umefanyika Senegal kwenye ubal… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni