Jumapili, 12 Februari 2017

40 ya Nillan: Wolper Achafua Hali ya Hewa, Atoa Povu Hadharani Mbele ya Wageni

WAKATI sherehe ya kutimiza 40 kwa mtoto wa Diamond na Zari, Nillan ikiendelea, staa wa Bongo Movies, Jackline Wolper Massawe amekerwa na wanaomsema vibaya Zari na kuamhua kuwafungukia hadharani akitoa povu lake mbele ya wageni waalikwa.

Baada ya Kutoka Selo Kwa Dhamana Hii Ndio Post ya Kwanza Aliyoandika Wema Sepetu Instagram


Inawezekana kama wewe ni shabiki wa Wema Sepetu ulikua na hamu sana ya kujua post yake ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii itahusu nini baada ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama kufuatia sakata la dawa za kulevya lililomfanya alale Polisi.

Post ya kwanza ya Mwigizaji huyu haijahusu chochote kuhusu kesi yake ama alichokipitia wiki iliyoisha bali imemuhusu dada yake ambaye leo ni siku yake ya kuzaliwa kama inavyoonekana hapa chini.



Wema Sepetu atarudi tena Mahakamani mwishoni mwa mwezi huu baada ya kupata dhamana Alhamisi ya wiki iliyopita kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam.

Tundu Lissu Abaini Mbinu Chafu kwa Chama Fulani Kuweka Mgombea Urais TLS..!!!


Mwanasheria Mkuu wa Chadema na mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama hicho, Tundu Lissu amezungumzia hatua yake ya kujitosa kuwania urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Mosi, Lissu amesema amepata msukumo kutokana na kauli ya rais John Magufuli kuwa kuna kampeni zimeanza za kumuondoa rais wa sasa wa TLS na zinaendeshwa na chama fulani ambacho kimeweka mgombea wake.
Pili, akasema Lissu ni kauli kuwa mawakili wanaotetea wauza dawa za kulevya nao wakamatwe wawekwe ndani.
“Sikuwa na mpango wa kugombea lakini the moment (wakati) aliposema, nikasema sasa nitagombea urais wa TLS,” amesema mbunge huyo.
Rais alitoa matamko hayo katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Sheria iliyofanyika mapema mwezi huu kwenye uwanja wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Lissu amesema TLS imepoteza mwelekeo na nafasi yake katika jamii kwenye masuala ya kisheria, hasa kushindwa kukemea vitendo vya uvunjifu na ukiukaji wa Katiba na sheria unaofanywa na viongozi.
“Chama cha wanasheria kinatakiwa kiwe cha kwanza kupiga kelele sheria za hovyo zinapotungwa, kinatakiwa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya ukiukaji wa Katiba na sheria vinavyofanywa na watu wenye mamlaka lakini Law society ya kwetu imekaa kimya,” amesema.
Kuhusu msimamo wake wa kisiasa na chama hicho endapo atapata nafasi hiyo, Lissu amesema masuala ya kisheria hayana uhusiano na vyama vya kisiasa na kwamba chama hicho kipo kwa ajili ya kulinda na kusimamia utawala wa sheria.
Pia, amesema kama chama chake kitakuwa na msimamo sawa na misingi ya chama hicho katika kutetea utawala wa kisheria, si tatizo na kwamba, ikiwa kitakuwa na msimamo tofauti katika mambo ya msingi, hakina budi kukosolewa.
“Sigombei ili kuipeleka Chadema ndani ya TLS. Masuala haya yanatuhusu sisi wote kujua mambo yanapoharibika, kuona sheria zinapokiukwa na kuona sheria mbovu zinapotungwa,” alisema.
Ofisa Maboresho ya Sheria wa TLS, Mackphason Buberwa amesema mchakato wa kupata wagombea umeshakamilika na waliopitishwa na kamati ni watano.
“Taratibu zimekamilika, kilichobaki ni wagombea kuandaa kampeni zao kabla ya Machi 18 siku ambayo uchaguzi utafanyika mjini Arusha,” amesema Buberwa.
Wagombea wengine ni Francis Stola, Lawrance Masha, Victoria Mandali na Godwin Mwapongo. Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Machi 18 jijini Arusha ambako zaidi ya mawakili 6,000 wanatarajiwa kuhudhuria.

Jaji Chande Apewa Kazi Umoja wa Mataifa..!!

Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande ameteuliwa kuongoza jopo la wataalamu watakaochunguza mazingira yaliyosababisha ajali ya ndege iliyomuua aliyekuwa katibu mkuu wa umoja huo, Dag Hammarskjold.
Uteuzi huo wa jaji mkuu mstaafu umefanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres.
Hammarskjold alipoteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokea Zambia mwaka 1961 wakati akitokea Congo ambayo ndiyo kwanza ilikuwa imepata uhuru.
Hammarskjold alikuwa nchini humo kwa ajili ya ujumbe wa amani.
Naibu msemaji wa UN, Farhan Haq amesema Chande ataongoza jopo hilo ambalo litakuwa na kazi kupitia taarifa zilizoandaliwa na wachunguzi waliopewa jukumu na katibu mkuu mstaafu, Ban Ki-moon.
Uchunguzi huo unafuatia azimio la Umoja wa Mataifa lililopitishwa na Baraza Kuu ambalo lilipendekezwa kufanyika uchunguzi wa kina kubaini mazingira ya ajali hiyo.
Awali, kulikuwa na ripoti kuwa Uingereza na Marekani zilikuwa zimegoma kutoa baadhi ya taarifa muhimu kuhusu tukio hilo, huku Afrika Kusini ikilalamikiwa kwa kushindwa kutoa majibu kwa baadhi ya hoja.
Ripoti iliyotolewa na wataalamu huru waliochunguza ajali hiyo inaeleza kuwa Hammarskjold aliuawa baada ya kunusurika kwenye ajali hiyo. Kumekuwa na taarifa kuwa ndege hiyo ilishambuliwa.
Jopo hilo linaloongozwa na Chande linatarajia  kuanza kazi mara moja na kwamba litakuwa na jukumu la kupitia nyaraka zote, ikiwamo ripoti ya kurasa 99 iliyoandaliwa na wataalamu wa awali waliochunguza mazingira ya ajali hiyo.

Vita Dhidi ya Madawa ya Kulevya..Wanawake Wawili Wadakwa na Kilo 114 za Bangi..!!


Wanawake wawili ni miongoni mwa watu zaidi ya 15 waliokamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya mkoani Mwanza
Watu hao wamekamatwa wakijihusisha nadawa hizo ndani ya wiki moja kuanzia Febuari 6.
Habari zinasema wanawake hao wamekamatwa wilayani Magu wakiwa na kilo 114.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema watuhumiwa 11 wamekamatwa wilayani Nyamagana na Ilemela na kilo 57 za dawa za kulevya aina ya miraa na kete mbili zinazodaiwa kuwa ni heroin.
“Mtuhumiwa mwingine ambaye ni mfanyabiashara wa vipuri vya magari, alikamatwa eneo la Butimba akiwa na kete 240 ya dawa za kulevya zinazodaiwa kuwa ni  heroin na ndunga mbili,” amesema.
Msangi amesema mtuhumiwa huyo alitaka kuzitumbukiza  chooni dawa hizo ili kupoteza ushahidi, lakini polisi waliwahi kukata bomba.

Alhamisi, 19 Januari 2017

Gambia bado kwa moto, Adama Barrow kaapishiwa Urais akiwa nje ya nchi

Adama Barrow ambaye ni mwanasiasa wa upinzani ambaye inaaminika ndie mshindi wa uchaguzi wa Urais Gambia ameapishwa kuwa Rais wa Gambia japokua uapisho wake umefanyika nje ya taifa hilo.
Uapisho umefanyika Senegal kwenye ubalozi wa Gambia ambapo raia wengi wa Gambia wanaofanya kazi Senegal wamehudhuria kuapishwa kwa Adama na hiyo imetokana na kugoma kuoachia madaraka kwa Rais Yahya Jameh na kutangaza hali ya hatari.

RAIS DKT MAGUFULI ATEUA MABALOZI SITA KUWAKILISHA TANZANIA NCHI MBALIMBALI