
SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limeeleza kuridhishwa kwake na utendaji wa Rais John Magufuli katika mapambano ya rushwa, kuongeza uwajibikaji na ukusanyaji wa mapato.
Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez, alisema hayo jana katika semina ya wabunge kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikipambana na rushwa na kusimamia kwa karibu ukusanyaji mapato, hali aliyosema itasaidia maendeleo kwa kuwa hakuna nchi iliyoendelea bila kuchapakazi.
Rodriguez alisema mbali na kuona maendeleo katika baadhi ya mikoa na mitaa, ameona jitihada hizo za Serikali na amefurahishwa na kuridhika nazo.
Mwakilishi huyo pia alisema Serikali ya Tanzania na Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN), zimekuwa zikifanya kazi pamoja katika harakati za usambazaji wa malengo ya dunia kwa Watanzania.
Alisisitiza umuhimu wa malengo hayo kueleweka kwa wabunge, ili katika jukumu lao la kuisimamia Serikali, wawe mabalozi wa utekelezaji wa malengo hayo katika ufuatiliaji kwenye ngazi zote za utawala.
Jumapili, 5 Juni 2016
UN WAKUNWA NA KASI YA JPM
Alhamisi, 12 Mei 2016
Mpinzani wa Museveni , Dr Kiiza Besigye Akamatwa Baada ya Kujiapisha Kuwa Rais
Mpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Museven kuapishwa.
Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa vizuizi vya polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.
Video hiyo ilisambazwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliopita akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wakuu, Kizza Besigye na Amama Mbabazi.
Kadhalika, Mahakama Kuu nchini humo ilihalalisha ushindi wa Museveni baada ya kutupilia mbali shauri la pingamizi la ushindi huo lililowasilishwa na Amama Mbabazi.
Viongozi Wakuu Wote wa Taifa Wako nje ya Nchi ..Nani Anaongoza Nchi Kwa Sasa?
Viongozi wakuu wote wa Taifa wako nje ya nchi katika ziara za kiserikali kwenye mataifa tofauti.
Rais John Magufuli aliwasili Uganda jana asubuhi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Yoweri Museveni zinazofanyika leo na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan alikuwa Kigali, Rwanda kuhudhuria mkutano wa dunia wa uchumi.
Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Mwandishi wa Makamu wa Rais, Penzi Nyamngumi zimesema, Makamu wa Rais aliondoka nchini Jumanne akitokea Dodoma na angerejea kesho baada ya mkutano huo.
Kiongozi anayefuatia kwa wadhifa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisafiri juzi kwenda London, Uingereza kumwakilisha Rais Magufuli katika mkutano wa wakuu wa nchi kujadili mapambano dhidi ya rushwa.
Majaliwa katika ziara hiyo ameongozana na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya anayepaswa kukaimu urais, alisema Makamu wa Rais amekwisha rejea nchini na yuko Mwanza.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 37 (3), inaeleza kuwa endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na Makamu wa Rais, kama naye hayupo, yatatekelezwa na Waziri Mkuu.
Hata hivyo, Ibara ya 37 (6) (b) inasema Rais hatahesabiwa kwamba hayupo iwapo atakuwa nje ya Jamhuri ya Muungano kwa kipindi cha saa 24.
Jumamosi, 7 Mei 2016
Serikali yakamata Tani 4,900 za Sukari iliyofichwa Mbagala na Tabata jijini Dar
Shetta Akanusha Taarifa Kuwa Diamond Amewahi Kutoka Kimapenzi na Mkewe
Shetta amekanusha taarifa zilizozagaa mitandaoni kuwa Diamond amewahi kutoka kimapenzi na mama Qayllah.
Wiki kadhaa zilizopita Shetta alifuta picha zote kwenye akaunti yake ya instagram huku akiwaacha mashabiki wake wakijiuliza maswali mengi kutokana na kitendo hicho.
Akiongea kwenye kipindi cha Leo Tena, kinachoruka kupitia Clouds FM, Shetta amesema, “kuhusu suala la mama Qayllah kutoka na Diamond hakuna ukweli wowote.”
“Kuhusu suala la kufuta picha ni management yangu mpya ilinishauri hivyo ndiyo maana unaona nilifuta picha zote hizo. Team team tu wameanzisha na kuzisambaza mitandaoni lakini hakuna ukweli wowote namuamini sana mke wangu. Mimi na Diamond tuko vizuri ila hizo,” aliongeza.
Kajala Ahusishwa Undani wa Wimbo wa ‘Haya Yote ni Maisha’ ya P Funk
Msanii Madee amefunguka undani wa wimbo wa ‘Haya Yote Maisha’ wa Producer P Funk Majani ambao ameimba yeye, wimbo ambao ulishika chati na kugusa hisia za watu wengi.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Madee amesema wimbo huo ni historia ya kweli ya P Funk na mwanamke ambaye ndiye mama wa mtoto wake wa kwanza, Kajala Masanja.
Madee aliendelea kusema baada ya mazungumzo P Funk alikubali kumpa beat na kwenda kuifanyia kazi, baada ya kukumbuka Madee mtindo alioutumia kwenye nyimbo zake.
“Haya yote maisha imetokea kipindi ambacho bado nipo na P Funk, alafu P Funk ana matatizo na mama mtoto wake Kajala, kwa hiyo wakati mi naenda pale kurekodi cheza kidogo, kabla sijamalizana na ile nakutana na beat ya yote maisha inaplay, alafu inaplay na chorus lakini hakuna verse, lakini the way ile beat inavyoplay majani anavyoiimba anaimba kwa feelings kinoma, nikamwambia bwana hii nyimbo mbona kali nigaie niimbe akasema hii na chana mwenyewe babu,” alisema Madee.
“Sema wewe ulivyochana kwenye kazi yake mola kuna ryhmes fulani naona unapita pita, unaongea kimajonzi hebu chukua hii beat kaandike, kwa hiyo nikapewa ile beat, aliniambia kwamba hii nyimbo ina feeling zangu, nataka uandike kitu hiki na hiki, kwa hiyo idea iliyotoka mule ni idea ya P Funk,” alisema Madee akimuongelea P Funk Majani.
Idadi ya Ajali zilizojitokeza wakati wa Majaribio Mabasi yaendayo Haraka
Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umesema kutozingatia sheria za barabara za mradi wa mabasi hayo, kwa vyombo vingine vya moto vimesabisha ajali 14 wakati madereva wa mabasi hayo wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya kuelekea kipindi cha mpito cha mradi kinachotarajia kuanza hivi karibuni.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Mhandisi Ronald Rwakatale amesema kuwa ajali hizo zimejitokeza wakati madereva wa mabasi ya mradi wakifanya mazoezi na kisha vyombo vingine vya moto viingilia barabara zake na kusabisha ajiali hizo.
Amesema ajali hizi ni matokea ya vyombo vingine vya usafiri kama magari madogo, daladala, bodaboda na waenda kwa miguu wamekuwa wakiingilia barabara za mabasi hayo na kusabisha ajali kutokana na kwamba barabara hizo haziruhusu mabasi hayo kupisha na vyombo vingine.
Mhandisi Rwakatale amesisitiza kuwa barabara za mabasi hayo ambazo ni za zege zimejengwa mahususi kwa ajili ya mabasi hayo hivyo madereva wa vyombo vingine wanahitajika kuheshimu sheria zinazoongoza mradi huo na kupita katika barabara walizotengewa na watakaokiuka sheria itachukua mkondo wake.
Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka unatarajiwa kuanza kipindi cha mpito mwezi huu wa Mei kutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam






