Mkuu
 wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akiongea na watoto 
wanaotoka katika vituo mbalimbali  vya kulelea watoto yatima vya  jijini
 Dar es salaam , wakazi wa jiji la Dar es salaam na viongozi mbalimbali 
wakati wa Futari aliyooiandaa jana usiku katika viwanja vya Karimjee.
Rais
 Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya
 Karimjee kuhudhuria Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es 
salaam Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kushoto) kwa watoto yatima 
kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es 
salaam. Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya 
Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es 
salaam Alhadi Mussa Salum.
Baadhi ya akina mama na watoto waliohudhuria Futari hiyo wakipata Chakula.






0 comments:
Chapisha Maoni