JUMLA ya Watanzania 578 wamekamatwa na kufungwa katika magereza ya nchi
mbalimbali kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Akiahirisha mkutano wa sita wa Bunge la 11 mjini Dodoma juzi, Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, alitaja nchi ambazo Watanzania hao wamefungwa kuwa
ni pamoja na China (200), Brazil (12), Iran (63), Ethiopia (7) na
Afrika ya Kusini (296).
Majaliwa pia alisema vita inayoendelea nchini dhidi ya dawa za kulevya inapaswa kuungwa mkono.
Alisema madawa ya kulevya huingia zaidi kutumia kwa njia za bandari bubu
kupitia Bahari ya Hindi na mipakani kwa njia ya magari binafsi na
mabasi yatokayo Kenya, Uganda na Zambia.
“Lengo la serikali ni kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya na
kuwachukulia hatua kali wale waliowaathiri - wauzaji na wasambazaji,"
alisema Majaliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni