ISHU hot iliyotrendi wiki hii ni kuhusu kigogo mmoja kudaiwa
kumpangishia Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ mjengo
wa maana uliopo Makongo Juu jijini Dar ambapo Ijumaa limechimba ili
kujua ukweli wa mambo.
Madai hayo yaliibuka juzikati baada ya watu kibao wakiwemo mastaa kuhoji
kwa nini modo huyo hakutajwa kwenye listi ya mastaa wa unga wakati
aliwahi kunaswa akisafirisha ‘mzigo’ nchini Afrika Kusini na sasa
anaishi maisha bomba.
“Unajua kati ya mastaa wanaoishi kwenye nyumba za kifahari Masogange
yumo, watu wanasema anauza madawa lakini ninachojua mimi ni kwamba
kapangishiwa bonge la jumba kule Makongo juu, ukifika pale utadhani
anaishi bosi f’lani.
“Kapangishiwa na kigogo mmoja na huyo ndiye anampa jeuri mjini, sasa
jaribuni kufuatilia mtaujua ukweli ila mimi msinitaje, msije
mkanitafutia matatizo,” alidai mtoa ubuyu huyo.
Kufuatia madai hayo, Ijumaa lilifanya jitihada za kufahamu ilipo nyumba
hiyo ambapo, kwa kuwatumia watu wanaomjua vizuri lilifanikiwa kufika
Makongo Juu na kushuhudia nyumba hiyo ya kihafari.
Katika ‘kunyapianyapia’ ili kujua kama staa huyo alikuwemo ndani,
paparazi wetu aligonga geti muda mrefu lakini halikuweza kufunguliwa
wala kuonekana mtu yeyote.
Ijumaa laamua kumpigia simu
Waandishi wetu wakiwa wamekaa nje ya nyumba hiyo huku wakiangaza huku na
kule, waliamua kumpigia simu Masogange na bahati nzuri alipokea na
alipoambiwa wako nje kwake, alijibu kuwa hakuwepo hapo nyumbani.
“Sipo, niko mbali kidogo,” alisema mdada huyo mwenye figa matata.
Alipotakiwa kufungukia madai kuwa, nyumba hiyo anayoishi amepangiwa na
kigogo mmoja maarufu na ndiye anayempa ujanja wa kuishi mjini, Masogange
alisema kuwa ni kweli amepangiwa nyumba hiyo lakini siyo na kigogo kama
inavyodaiwa.
“Watu wanasema eti nimepangiwa nyumba na kigogo, ukweli naujua mwenyewe.
Nina mpenzi wangu na ndiye aliyenipangishia nyumba hii na hili suala
lipo wazi kabisa kwani watu wangu wa karibu wanamjua,” alisema
Masogange.
Aidha, katika muendelezo wa madai ya Masogange kupangiwa mjengo na
kigogo, juzikati ilivuja clipu iliyodaiwa ni ya staa Wema Sepetu akihoji
sababu za Masogange kutotajwa kwenye listi ya mastaa wa unga.
Hata hivyo, juzi kwenye mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na
waandishi wa habari, mmoja wa mapaparazi alimuuliza sababu za Masogange
kutotajwa kwenye listi hiyo kama alivyodaiwa kuhoji Wema ambapo
mheshimiwa huyo aliyedhamiria kupambana vilivyo na biashara ya madawa ya
kulevya katika Jiji la Dar alijibu:
“Kwanza ni kosa kisheria mtu anapokuwa anashikiliwa na jeshi la polisi
kushika simu, sasa kama una jambo unataka kulisema na uko polisi, kwa
nini usiliseme badala yake u.”
0 comments:
Chapisha Maoni