Jumatatu, 2 Mei 2016

Baada ya Kutoka Marekani Mtoto Getrude Clement Akaribishwa Bungeni Leo

Getrude Clement mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza, leo amepata nafasi ya kufika bungeni Dodoma baada ya kupewa mwaliko wa Serikali
Hivi karibuni Getrude alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika New York Marekani ambapo leo Bungeni amewahimiza Watanzania kutunza mazingira na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.
Getrude amesema kuwa amefarijika kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana kusaini makubaliano ya Paris.
Katika kuwahimiza vijana kujenga tabia ya kutunza mazingira, Getrude amewaasa vijana hasa wanafunzi kusimamia suala la utunzaji wa mazingira wakiwa shuleni kwa kwa kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na klabu ya “Mali Hai” iliyopo shuleni anaposoma.
Kwa upande wa Watanzania kwa ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude amesema kuwa ni vema wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia utunzaji wa mazingira hasa matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mwanafunzi huyo amekaribishwa na kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa heshima ya kuliwakilisha vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao na kusema “Ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana”.


Related Posts:

  • Breaking Rapper Geez Mabovu amefariki dunia usiku huu  Kabla mwaka 2014 haujaisha idadi ya watu maarufu wa Tanzania waliotangulia mbele za haki imezidi kuongezeka na hii ni baada ya taarifa kutoka Iringa zilizoanza kusambaa kuanzia saa tatu usiku November 11 2014. Taari… Read More
  • Taarifa kuhusu ajali ya moto ulioteketeza shule ya msingi. Hii sio picha halisi ya ajali ya moto huo. Moto mkubwa umeteketeza majengo ya Shule ya msingi Filbert Bayi na kisha kusambaa na kuteketeza mabweni yote ya Wanafunzi pamoja na madarasa. Mwenyekiti wa shule hiyo Filbert … Read More
  • Rais Goodluck kugombea tena urais  Rais Goodluck amekuwa akikosolewa kwa mamna anavyoshughulikia swala la Boko Haram Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amethibitisha rasmi kuwa atagombea tena kiti hicho mwaka ujao. Katika sherehe ya kufana katika mji … Read More
  • HATMA YA AFCON 2015 ? Shirikisho la soka barani afrika CAF limewaondoa mashindanoni waliokuwa wenyeji wa michuano ya AFCON Morocco baada ya taifa hilo kushikilia msimamo wake wa kutokuwa tayari kuandaa michuano ya AFCON mwaka 2015 kutokana na… Read More
  • Tanzania vs Uganda katika Kickboxing. Mtanzania anayefanya vizuri kwenye mchezo wa kickboxing Emmanuel Shija hivi karibuni ataipeperusha bendera ya Tanzania nchini Uganda wakati atakapopanda ulingoni kupambana na  Mganda Moses Golola katika pambano la … Read More

0 comments:

Chapisha Maoni