Mgombea mkuu wa chama cha Republican Donald Trump ameshutumu Uchina na kusema imekuwa “ikiibaka” Marekani kupitia sera zake za kibiashara.
Ameambia watu waliohudhuria mkutano wa kisiasa Indiana kwamba Uchina imekuwa ikitekeleza “wizi mkubwa zaidi kuwani kutekelezwa katika historia ya dunia.”
Bw Trump, mfanyabiashara tajiri kutoka New York, amekuwa akiituhumu Uchina kwa kuchezea sarafu yake ili kuwa na ushindani wa kibiashara duniani inapouza bidhaa nje ya nchi.
Hilo, amesema, limeathiri sana wafanyabiashara na wafanyakazi wa Marekani.
“Hatuwezi kuruhusu Uchina iendelee kuibaka nchi yetu, na hilo ndilo tunafanya (kwa wakati huu),” alisema mkutanoni Jumapili.
"Tutabadilisha mambo, na tuna uwezo, msisahau. Tuna nguvu sana dhidi ya Uchina.”
Katika manifesto yake ya kampeni, Bw Trump ameahidi kufanikisha mkataba bora wa kibiashara baina ya Uchina na Marekani ambao utawezesha “wafanyabiashara na wafanyakazi kutoka Marekani kuweza kushindana”.
Obama: Trump haelewi sera za kigeni
Ametaja malengo manne ambayo yanahusisha kutangaza Uchina kuwa taifa linalochezea sarafu yake na kusitisha utoaji wa nafuu za wafanyabiashara wanaouza bidhaa nje ya nchi ambazo anasema ni haramu.
Aidha, anaitaka Uchina kufikisha kikomo mfumo duni wa masharti ya leba na uhifadhi wa mazingira.
Takwimu za karibuni zaidi kutoka kwa serikali ya Marekani zinaonesha pengo la kibiashara baina ya Uchina na Marekani lilipanda na kufikia $365.7bn (£250.1bn) mwaka jana. Kufikia Februari mwaka huu, pengo hilo lilikuwa limefika $57bn tayari.
Hii ni mara ya kwanza kwa Trump kutumia neno “ubakaji” akizungumzia biashara na Uchina, lakini amejulikana kwa kutumia maneno makali kwenye kampeni yake.
Alikabiliwa na mamia ya waandamanaji jimbo la California Ijumaa kabla yake kutoa hotuba katika mkutano wa chama cha Republican Ijumaa.
Alilazimika kutumia mlango wa nyuma kuingia.
Waziri mkuu wa Uchina Li Keqiang amesema Wachina wanafuatilia kwa karibu uchaguzi nchini Marekani.
Hata hivyo anasema wengi wanamtazama Bw Trump kama mtu wa kuenziwa badala ya adui.
Jumatatu, 2 Mei 2016
Home »
» Donald Trump Asema Uchina “inaibaka” Marekani
Donald Trump Asema Uchina “inaibaka” Marekani
Related Posts:
Man U na Arsenal zawika,Chelsea yazuiwa Mchezaji wa chelsea Wiilian akikabiliana na mwenzake wa Sunderland Mkufunzi Gus Poyet aliihangaisha timu ya Chelsea na kuwajaribu viongozi hao wa Ligi kupi… Read More
Walichokisema Wabunge Kafulila, Peter Msigwa, Aeshi Hilary na Maige kuhusu maamuzi ya Bunge jana Kikao cha Bunge la Tanzania kilichoahirishwa siku ya jana Novemba 29 ni moja ya vikao ambavyo vilivuta hisia za watu wengi na kutengeneza historia nyingine mpya kutokana na mjadala wa ishu ya Escrow, baada ya kikao hich… Read More
FIFA:Madai mapya ya ufisadi yazuka Rais wa FIFA Sepp Blatter akimkabidhi rais wa Urusi Vladmir Putin Haki za kuandaa dimba la dunia la mwaka 2018 Madai zaidi yameibuka kuhusu ufisadi uliofanyika wakati wa shughuli ya kuwatafuta waandalizi wa … Read More
ESCROW:Spika adaiwa kuwalinda washukiwa Spika wa bunge la Tanzania Anne Makinda Speaker wa Tanzania Anne Makinda ameshtumiwa kwa k… Read More
Maneno 6 ya Davido baada ya ushindi wa Diamond Platnumz Channel O 2014. Ushindi wa tuzo tatu za Channel O 2014 alizochukua Mtanzania Diamond Platnumz umekua mkubwa sio tu kwa Tanzania bali Afrika na kona zake ambapo miongoni mwa walioandika baada ya Diamond kushinda ni Davido. Msanii… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni