Serikali inaendelea kusimamia mazingira na kuhakikisha mifuko ya plastiki inayotumika nchini iwe ni ile inayokidhi viwango vianavyokubalika ili kuondokana na changamoto ya kuzagaa kwa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba alipokuwa akitoa hoja ya wizara yake kuidhinishiwa maombi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Makamba amesema kuwa sababu kubwa ya kusambaa kwa mifuko ya plastiki inatokana na mifuko hiyo kutolewa bure na hivyo kuchafua mandhari na kuziba mifereji sehemu mbalimbali hali inayosababisha athari kubwa katika mazingira.
“Asilimia kubwa kwenye mito, maziwa na fukwe za bahari imejaa mifuko ya plastiki, hali hii ni hari kwa usalama wa mazingira yetu” alisema Makamba.
Akiwasilisha hotuba yake, Waziri Makamba amesisitiza kuwa mifuko ya plastiki isiyotakiwa kutumika nchini ni ile yenye unene chini ya maikroni 50 ambayo hairuhusiwi kuzalishwa wala kuingizwa.
Kwa mujibu wa maelekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016, Waziri huyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imekamilisha kanuni mpya ya mifuko ya plastiki zinazorekebisha viwango vya unene unaoruhusiwa kutoka Maikroni 30 kwenda Maikroni 50.
Waziri Makamba amesema kuwa kanuni hizo tayari zimesainiwa kupitia tangazo la Serikali Na.271 la mwaka 2015 na kutolewa katika Gazeti la Serikali Julai 17, 2015 na kupewa Na. 29.
Jumatatu, 2 Mei 2016
Home »
» Waziri Makamba Awasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
Waziri Makamba Awasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
Related Posts:
MSUMBIJI: Mwanamke wa Kitanzania Abakwa Mpaka Kufa. Serikali Imefungwa Pasta? Jamani, Hii inasikitisha sana tangu kuanza kusikika kwa sakata la watanzania kufurushwa uko msumbiji mengi yametokea lakini serikali yetu inaonesha kuwakandamiza watanzania kuwaonesha hawakuwa wakiish kihalali kabis… Read More
Issue ya Masogange Kushikiliwa na Polisi ka Kuhusika na Madawa ya Kulevya, Uwoya Amlipua Wema...!! Lile sakata la masogange kuwekwa ndani kwa shutuma za madawa ya kulevya, limeingia ukurasa mpya baada ya hivi karibuni rafiki wa masogange ambaye pia ni staa wa filamu aitwaye Irene uwoya, kumjia juu wema sepetu baa… Read More
Baada ya Kumuita Nyani, Iyobo Amvaa Tena Harmorapa...!!!! KIONGOZI wa madansa ambaye ni dansa tegemezi wa Wasafi Classic Baby (WCB) Mose Iyobo amefunguka kuwa yeye hana imani na Harmorapa na anashangaa anavyotajwa kila mahali kwani yeye hajawahi kusikia kazi yake yoyote hi… Read More
Ulimi Kisimini-Siri Ya Mwanamke Kufika Kileleni. Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa tendo) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa w… Read More
Uwoya ni Gusa Unate..!!!! Msanii maarufu wa filamu Bongo, Irene Uwoya (pichani) anatajwa kuwa kati ya mastaa wa kike Bongo aliyewahi kutoka na mastaa na vigogo mbalimbali huku ikidaiwa kuwa, kila aliyekuwa naye alimuacha yeye na si kua… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni