Boss wa Leicester City Claudio Ranieri anauwezekano mkubwa asiangalie mechi ya Chelsea na Tottenham hii leo kwa sababu atakuwa ndani ya ndege kutoka Italia.
Mbweha hao weupe kutoka Kings Power watachukua ubingwa Premier League kama Tottenham itashindwa kuifunga Chelsea ugenini Stamford Bridge leo.
“Ningependa kuangalia mechi ya Tottenham lakini nitakuwa kwenye ndege natokea Italia,” Alisema Ranieri. “Mama yangu ana umri wa miaka 96 na napenda kula naye chakula cha mchana leo kabla sijarudi Uingereza kwa hiyo nitachelewa.”
Kocha huyo raia wa Italia hajawahi kushinda taji la ligi katika kazi ya ukocha, lakini Leicester ina kila dalili ya kumpa nafasi hiyo ikiwa hadi sasa inahitaji pointi mbili tu ili kutangaza Ubingwa kufuatia sare yao ya 1-1 na Manchester United hapo jana.
“Katika mawazo yangu, Tottenham itashinda mechi zote tatu, “ alisema. “Mimi nafikiria mechi dhidi ya Everton ni lazima tuendelee kucheza kwa makini ili tuendelee kushinda. “
Jumatatu, 2 Mei 2016
Home »
» RANIERI KUIKOSA MECHI YA CHELSEA NA TOTTENHAM
RANIERI KUIKOSA MECHI YA CHELSEA NA TOTTENHAM
Related Posts:
FROLA MBASHA AKIRI MWANAE SI WA EMMANUEL MBASHAOHOOO! Kimenuka tena. Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amesema mwanaye mdogo (jina linahifadhiwa) hahusiani hata kidogo na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha huku akidai kuwa anamtambua mwanaume huyo kama mzazi mw… Read More
DR MTIKILA ALIUAWA KABLA YA AJALI DP MAPYAA! Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrati (DP), Abdul Juma Mluya ameibuka na kusema mazingira ya kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mchungaji Christopher Mtikila yamejaa utata huku akiweka wazi kwamb… Read More
MADUKA YA UCHUMI SUPERMARKET YAFUNGWA TANZANIA NA UGANDA Uongozi wa Uchumi Supermarket umetangaza kufunga shughuli zake katika maduka yake yaliyopo Tanzania na Uganda ili kutoa nafasi ya kuzuia mtikisiko wa kifedha unaoikumba kampuni hiyo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk Jul… Read More
MWANASIASA MKONGWE MZINDAKAYA AFUNGUKA MAKUBWA KUHUSU CCM NA WALIOHAMA MWANASIASA mkongwe nchini, Chrisant Mzindakaya amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wagombea wao wa nafasi mbalimbali, wasigombane na waliohama chama hicho kwa kusisitiza kwamba wakifanya hivyo, watakuwa… Read More
KILA KITU AANIKA:HATIMAYE AGNESS MASOGANGE AFUNGUKIA PENZI LA DAVIDO VIDEO Queen mwenye umbo tata Bongo, Agness Jerald ‘Masogange’ alifungukia penzi lake na staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido. Akizungumza na Amani Masogange alisema kuwa kuna uvumi unaovumishwa na baadhi ya watu kwamba a… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni