Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Mstahiki Boniface Jacob amezua taharuki kwa wamachinga wa ubungo na kukimbia biashara zao wakiambatana naye mithili ya Maandamano mara baada ya kutangaza kufuta umiliki wa vizimba na mabanda takriban 100 yaliyokuwa yakimilikiwa na watendaji na Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni katika soko la Mawasiliano Maarufu kama Simu 2000 akiagiza wapewe bure.
Mstahiki Jacob aliyefuatana na watendaji wa Manispaa hiyo alitembea kwa miguu akiongea na wamachinga mmoja mmoja na makundi kuanzia Ubungo Plaza hadi ubungo maji akiwaelimisha umuhimu wa oparesheni ya kuwaonda barabarani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa njia za juu na kuanza kwa usafiri wa mabasi ya kasi Dart ambao hali ilibadilika pale alipotaja Manispaa kuwa na masoko 26 yaliyohodhiwa na viongozi kwa kuingia Mikataba ya kupangisha wakati wamejiagawia bure.
Aidha Mstahiki Meya Boniface Jacob amesema katika kuhakikisha wafanya biashara wadogo wanatengewa maneo yao watafanya uhakiki katika masoko yote kubaini viongozi na watendaji waliojimilikisha na kuwanyang’anya ili masoko yatumiwe na walengwa ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya jiji huku mtendaji wa kata ya ubungo Bw. Gilbati Mushi akieleza hatua hiyo kudhirisha utawala bora.
Jumatatu, 2 Mei 2016
Home »
» Meya wa Kinondoni Agawa Bure Maeneo ya Biashara Leo na Kufuta Umiliki wa Vibanda na Vizimba 100
Meya wa Kinondoni Agawa Bure Maeneo ya Biashara Leo na Kufuta Umiliki wa Vibanda na Vizimba 100
Related Posts:
HUYU NDO MKE WA MAREHEMU MBUNGE DEO FILIKUNJOMBE ALIYE FARIKI KWENYE AJALI YA HELIKOPTA YA CCM Huyu Ndo Mke wa Marehemu Mbunge Deo Filikunjombe Aliyefariki Kwenye Ajali ya Helkopta ya CCM … Read More
P-square na Fally Ipupa Walitamani Kuwachukua Dancers wa Diamond Dancers wa P-Square pamoja na msanii mkubwa wa nchini Congo, Fally Ipupa walijaribu kumshawishi Diamond ili wafanye kazi ya pamoja na dancers wake. Akizungumza na Bongo5 jana mmoja wa dancers hao, Imma Platnumz, alisema … Read More
PICHA ZA MABAKI YA HELIKOPTA ILIYOPOTEZA UHAI WA MBUNGE DEO FILIKUNJOMBE Mwili wa Deo Filikunjombe ukitolewa Eneo la tukio baada ya kuteketea kwa Moto kufuatia ajali ya helkopta. Waliofariki mbali ya Filikunjombe wengine ni Mwenyekiti wa TLP Mkoa wa Iringa Blanka Francis Haul… Read More
MWANAMUZIKI ALI KIBA ATOA WIMBO MPYA...USIKILIZE HAPA JINA LA WIMBO MAUMIVU Huu ni wimbo mpya wa msanii Ali Kiba ambao umevuja unaitwa “Maumivu” Producer: Manecky … Read More
BAADA YA KUJITOA CCM BAKOZI JUMA MWAPACHU ATOA MPYA..ADAI HATA NYERERE ANGEKUWEPO ANGEJITOA CCM Siku moja baada ya kutangaza kujitoa CCM, kada mkongwe wa chama hicho, Balozi Juma Mwapachu amesema uamuzi alioufanya ni sahihi ambao hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere angekuwa hai angeufanya kwa sasa. Balozi M… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni