Januari 29, 2009 Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda alimwaga machozi Bungeni na kufikia hatua ya kutoa kauli kali juu ya wanaofanya vitendo vya kikatili vya mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwamba “wanaoua albino nao wauawe”
Hadi sasa idadi ya Watanzania wanaosubiri kunyongwa imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na kufikia 465 kutokana na hukumu ya kifo kutotekelezwa nchini tangu mwaka 1994.
Ripoti ya Mpango wa Kujitathmini Kuhusu Hali ya Utekelezaji wa Haki za Binadamu (UPR), unaotekelezwa kwa mara ya pili nchini Tanzania, umeonesha ongezeko la mahabusu 465 wanaosubiri adhabu ya kifo, kati yao wanaume ni 445 huku wanawake wakiwa 20 baada ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kubainisha hakuna hukumu yoyote ya kifo iliyosainiwa na Rais Dk. Magufuli ili kutekelezwa tangu Oktoba mwaka jana alipoingia madarakani.
Hata hivyo Ofisa Uchunguzi Mkuu wa Tume hiyo Philemon Mponezya, amesema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, inaitaka Serikali kufuta adhabu ya kifo kwa kuwa haitekelezeki ingawa kumekuwa na mvutano mkali kati yao na baadhi ya asasi hasa zinazohusika na haki za walemavu wa ngozi zikipinga vikali kufutwa kwa adhabu hiyo.
“Watetezi wengi wa haki za binadamu nchini Tanzania wanataka adhabu hiyo ifutwe kwa kuwa ni kinyume cha haki za binadamu na kwa Tanzania, imekuwa mbaya zaidi kwa baadhi ya wahukumiwa waliosubiri zaidi miaka 20 bila hukumu dhidi yao kutekelezwa, jambo hili linawaathiri kisaikolojia”. Amesema Mponezya.
Jiunge nasi
Insta@ubuyuhotz , fb@ubuyuhotz .
Jumapili, 1 Mei 2016
Home »
» IDADI YA WANAOSUBIRI KUNYONGWA TANZANIA YAONGEZEKA
0 comments:
Chapisha Maoni